Frank Mtao ambae amedaiwa kumpa taraka mkewe Chuchu Hans kisa rafiki yake Ray
Ni kipindi
kirefu sasa kumekuwa na madai ya kashfa ya msanii Vicent Kigosi “Ray “ kudaiwa
kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa
mtu ambae pia ni msanii wa bongo muvi Chuchu Hans huku vyombo mbalimbali vya
habari hasa magazeti pendwa yakiripoti kwa kina tukio hilo.
Habari za
ziada zilizonaswa toka kwa mtu wa karibu na familia ya Frank Mtao
zilisema kuwa taarifa za Ray kutembea na Chuchu Hans zinaukweli kubwa sana
kwani hata tukio la hivi karibuni la Ray kufumaniwa na akiwa na Chuchu Hans
wanazichukulia kama ni za ukweli kwani Johari ambae ndiye mchumba harisi wa Ray
aliwahi kukutana na mmoja wa wanafamilia wa Frank Mtao na kuwaeleza kila kitu.
Hata hivyo Ray kwa inadaiwa kusababisha ndoa ya Frank
Mtao kuvunjika kwani hivi karibuni Frank Mtao ambae anaishi nchini Austaralia
baada ya tukio la kufumaniwa mkewe na Johari akiwa na Ray nyumbani kwa Chuchu
mtangazaji huyo amemtwanga taraka Chuchu Hansa ambae sasa hivi maisha
yanamwendea kombo baada ya kushindwa kulipia pango ya nyumba maeneo ya Msasani
na kuhamia Mwananyamala kwa Mama Zacharia uswahili.
Aidha katika hali isiyokuwa ya kawaida Ray amekuwa
akimng’ong’a Frank Mtao kwa kujifanya kuwa ni rafiki yake wa karibu na mara nyingi amekuwa akimpigia simu Frank
Mtao na kumuweka roud speak wakati akiwa na Chuchu Hans.
Chanzo hicho
kiliendelea kueleza “ Kwa kweli inasikitisha kuna siku Ray alikuwa na Chuchu
Hans alimpigia simu Frank Mtao na kuanza kutaniana nae na baadae alimuuliza
kama huko hana demu hali na Frank alimjibu kuwa anae wa kuzugia na Ray
alihitaji Frank amtumie picha yake na Frank alifanya hivyo na picha hiyo
aliiona Chuchu Hansa na baadae palizuka mtiti mzito” Alisema dada huyo ambae
alisema yeye ni binamu wa familia ya Frank.
Aidha watu
mbalimbali wameonesha wasiwasi wao kuwa huenda Frank Mtao akalipa vibaya kwa
kumsomea alalbadir msanii Ray na kama kweli tuhuma anazotuhumiwa zitakuwa za
kweli msanii huyo atakuwa amejipatia matatizo makubwa kutokana na dua hiyo
jinsi inavyofanya kazi kama tukio lina ukweli na huenda akashushwa “busha” na
baadae kulazimika kutembea na mkwangwaju.
No comments:
Post a Comment