Monday, 9 September 2013

MZUNGU WA AFRIKAN BARRICK GOLD ATIWA MBARONI KWA KUMTELEKEZA MTOTO ALIYEZAA NA BINTI WA KITANZANIA.


Andre akiwa na mzazi mwenzie akimsihi aondoe shauri hilo
 mahakamani
 
Andre akiwa na mtoto wake nje ya mahakama
ANDRE LAPIERRE (50) MFANYAKAZI WA MGODI WA
BULHYAHULU 
 Mzungu akitoka kusikiliza shauri lake chumba cha mahakama ambapo shauri hilo liliahirishwa mpaka tarehe 4.10.2013 ambapo alidhaminiwa na wadhamini wawili .
 
Raia wa nchini Canada ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya African Barrick Gold Bulyanhulu aliyefahamika kwa jina la Andrew Lapierre (50) amefikishwa mahakama  ya mwanzo Lunguya wilayani kahama mkoani shinyanga kwa kosa la kutelekeza mtoto kinyume cha kifungu namba 166 cha sura ya 16 aliyezaa na Bi Elizabeth John.

Akisoma makosa ya mtuhumiwa, hakimu wa mahakama ya mwanzo Lunguya Derick Masaga ameiambia mahakama  kuwa Andre Lapierre  mwaka jana alimpa hujauzito Elizabeth John (21) mkazi wa Kakola ambaye alizaa mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Mariam Andre, na kumtelekeza muda wote bila huduma.

Mtuhumiwa  alikana kumtelekeza mtoto huyo na kuiomba mahakama hiyo iagize wakapimwe vipimo vya vinasaba (DNA) ili kubaini ukweli na vipimo vimethibitisha hilo.

No comments:

Post a Comment