Wednesday 30 October 2013

BAADA YA KASHFA YA KUPIGANIA PENZI LA RAY CHUCHU ATIMKIA INDIA


BAADA mwigizaji Chuchu Hans kukwaa skendo ya kupigania penzi la Vincent Kigosi ‘Ray’ na mwenzake Blandina Chagula ‘Johari’, amedaiwa kutimkia nchini India wikiendi iliyopita kwa lengo la kupunguza stress.

Habari zilizopatikana kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni shosti wa karibu na msanii huyo, zinasema tangu skendo hiyo iliporipotiwa magazetini, amekosa amani na amekuwa mtu wa kujificha sana. 


“Amekwenda kwa shangazi yake India, amesafiri wikiendi hii kwa ndege ya Emirates, tena ili kukwepa macho ya watu ameondokea Zanzibar. Ile skendo imemchanganya sana,” alisema shosti huyo akiomba asitajwe gazetini.

No comments:

Post a Comment