ipimo
Tikiti la asali (honey melon) 1
Unga wa embe au embe 1
Tangawizi 1 Kijiko
Ndimu 1
Sukari ¼ Kikombe cha chai
Arki rose 2 Matone
Namna Ya Kutayarisha
- imenye melon na ulikate kate kisha tia kwenye blender
- Tia unga wa embe au embe iliyokatwa katwa
- Kisha tia ndimu iliyokatwa vipande kiasi pamoja na maganda yake
- Halafu weka sukari
- Saga vizuri hadi ilainike
- Mimina kwenye jagi kisha tia matone mawili ya arki rose ukoroge na tayari kwa kunywewa
Kidokezo
Ukiweka ndimu weka na maganda yake unapata ladha nzuri zaidi.
No comments:
Post a Comment