Watu
wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tumbo lisilo la vidonda wala ugonjwa
wowote ila utasikia anakwambia tumbo linanikata, huenda akawa
anavurugikwa na tumbo au imetokea linasumbua tu.
Tiba hii hapa
Kwanza kabisa kama wewe unapenda kutumia vinywaji vikali ‘Alcohol’,
kahawa na vinywaji vyote vyenye ‘Caffeine’ jitahidi kuacha kwani inaweza
kuwa sababu ya wewe kusumbuliwa na tumbo.
Lakini kama tumbo ni
ugonjwa unaokusumbua mara kwa mara, kwanza chunguza katika hospitali
kuhakikisha huna tatizo kubwa la kutibiwa kabla ya kujipa huduma za
kinyumbani ‘Natural Remedies’.
Lakini ukishagundua huna tatizo kubwa huduma ya kwanza unayoweza kufanyiwa nyumbani ni hii hapa.
Kunywa chai yenye mchanganyiko wa Tangawizi, ‘chamomile’ na majani ya nanaa.
Limao
nayo inasaidia, unaweza kukatakata vipande na kunyonya maji yake kama
unavyokula chungwa, au unaweza kuweka kwenye glasi ya maji ya vuguvugu
na kunywa.
Kula Yogurt
Kula maziwa aina ya yogurt, haya yanasaidia kuliweka sawa tumbo lako
hasa pale linapokuwa kwenye hali ya kuvurugika. Kwa kufanya hivyo
unaweza kusafisha kwa kutoa uchafu tumboni au kukata kwa maumivu tu.
Hapa kwenye yogurt epuka yenye sukari nyingi jaribu kula yenye ladha ya
vanilla ni nzuri zaidi, kumbuka kinywaji hiki kina tibu mambo mengi
kwani mbali na tumbo pia husaidia kutibu msongo wa mawazo na kuweka sawa
akili
Tangawizi pekee
Chukua tangawizi isage kamua maji yake kisha weka kwenye kinywaji chochote chaweza kuwa cha baridi au cha moto ni dawa pia.
Epuka kula vyakula vizito usiku mwingi
Vyakula
hivyo husababisha tindikali kwenye tumbo na hufanyika pale usiku
unapokula haraka na kupanda kitandani bila kukipa nafasi chakula
kuyeyuka tumboni.
Kumbuka wakati mzuri wa kula chakula ni kati ya
saa mbili usiku mpaka saa nne na baada ya hapo usipande kitanda wakati
huohuo jaribu kujipa nafasi kwa ajili ya kuruhusu chakula kifike eneo
husika na kianze kusagwa ndiyo ulale.
Wengine hufanya zoezi la kutembea baada ya chakula ili kukipa nafasi nzuri ya kufanya kazi.
Utakuta mtu anakula viazi au wali maharagwe na jamii ya vyakula vingine
vizito kisha hajipi muda wala hanywi maji anadandia kitanda kisa
amechelewa kulala, hii ni sumu ndani ya tumbo lako kwani nafasi ya
kufanya kazi inakuwa ndogo sana.
No comments:
Post a Comment