Mambo vipi? Natumani kwamba
muwazima kabisa na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku. Mimi
namshukuru Mungu kwani amekuwa akinipa nguvu ya kuandika haya
ninayoamini yana manufaa kwenu.
Ndugu
zangu, ili uweze kudumu katika uhusiano wako unatakiwa kujenga
mazingira ya kumuamini sana mpenzi wako. Nasema hivyo kwa kuwa, mapenzi
ni imani. Ni sawa na kuamini Mungu yupo licha ya kwamba hujawahi
kumuona.
Vivyo
hivyo, amini tu kwamba mpenzi wako anakupenda kwa dhati licha ya kwamba
hujaufungua moyo wake na kathibitisha kwamba ndani yake uko wewe peke
yako.
Mpende,
muamini na weka akilini mwako kwamba, kamwe hawezi kukusaliti licha ya
kwamba kinyume chake pia ni sawa. Hiyo itakusaidia wewe kuendelea kuishi
maisha ya furaha na amani bila kuwa na presha.
Jiulize,
ni wanaume wangapi ambao wake zao wanagawa penzi nje ya ndoa lakini wao
wanawaamini kupita maelezo? Ni wanawake wangapi ambao waume zao ni
viwembe kwelikweli lakini wanawaamini kupindukia? Unadhani ni kwa nini?
Ni kwa sababu wamejijengea mazingira ya kuwaamini wenzao wao wa kiwango
kikubwa na kuziba masikio yao kukwepa wambeya.
Tutambue
tu kwamba, katika maisha kuna kitu kuridhika. Unapokuwa na mtu ambaye
anakupa kila aina ya furaha maishani mwako bila kuonesha tabia zozote
zinazokutia mashaka juu ya penzi lake, huyo mpende, mheshimu na muamini.
Hata
kama kuna uwezekano wa yeye kuwa anaficha makucha yake na kuyachomoa
pale anapokuwa mbali na wewe, kwa sababu huna uhakika na hujawahi
kumuona, chukulia kwamba yeye ni msafi kisha yaache maisha yenu
yaendelee kuwepo.
Nasema
hivyo kwa sababu, tukianza kuchunguzana hakuna ambaye ni msafi kwa
asilimia mia moja. Kila mtu anajiamini mwenyewe lakini huwezi kuiamini
nafsi ya mwenzako kwa asilimia zote.
Ndiyo
maana nikasema, unapoingia katika uhusiano na mtu ambaye umetokea
kumpenda sana, ongea na moyo wako. Moyo wako ndiyo utakueleza kama
mpenzi wako ni muaminifu ama siyo na pindi utakapoona dalili za kwamba
ni tapeli wa mapenzi mwenye lengo la kutaka kukuchezea kisha kukuacha
solemba, usimng’ang’anie eti tu kwa sababu umeoza kwake, muache!
Tatizo
tulilonalo wengi ni kutokuwa tayari kuwakosa wale ambao tumetokea
kuwapenda sana bila kujua kwamba unaweza kutokea kumpenda mtu lakini
yeye akawa hana mapenzi ya dhati moyoni mwake dhidi yako. Ifike wakati
tukubaliane na uhalisia kwamba, unapoona uliyenaye anakuzingua, yupo
mwingine mwenye penzi la dhati kwako ambaye anasubiri umuache huyo
uliyenaye ili awekeze penzi lake kwako.
Kwa
kumalizia naomba niseme kwamba, mapenzi ya siku hizi usipoangalia
yanaweza kukufanya ukawa chizi. Hii ndiyo inayosababisha baadhi ya watu
kufikia hatua ya kusema kwamba, hawahitaji kuwa na wapenzi katika maisha
yao. Kwa nini? Kwa sababu kila uhusiano wanaoingia wanakutana na
usanii.
Elewa
kwamba, una haki ya kupenda na kupendwa, ukishampata yule unayedhani
atayafanya maisha yako kuwa ya furaha, mpende kwa dhati na muamini
kwamba hawezi kukusaliti lakini, wakati huo hutakiwi kubweteka, chunguza
nyendo zake na kama utabaini kwamba anajiheshimu, ongeza mapenzi kwake
lakini kama utabaini kuwa hajatulia, muache.
No comments:
Post a Comment