Kila upande unatakiwa kuwajibika
Kuna
wanaume ambao kwa kutokujua wanadhani mwanamke anachohitaji ni ‘fidia’
baada ya kuvunjiwa heshima, hivyo huwa wanawavunjia heshima wake zao na
baadae kujitoza ‘fidia’ kwa kuwanunulia zawadi kubwakubwa wanawake hao.
Wanawake
huwa wanapokea zawadi hizi, lakini hii haina maana kwamba ndoa
itaendelea kuwa ya amani na upendo. Mwanamke hata kama atapewa dhahabu
yote duniani, kama atajua kwamba mumewe hamheshimu, ni wazi kwamba
hatakuwa na furaha ya ndoa. Miongoni mwa mambo sita ambayo mwanamke
akiyakosa huhisi kutindikiwa na kukosa furaha ya uhusiano ni heshima.
Kama
haki ya mwanamke hailindwi na mwanaume, hata kama kuna kitu gani, ndoa
ni lazima itakuwa ni ya kubahatisha. Mwanume anapokuwa na uhusiano wa
kipapenzi nje ya ndoa yake, mwanaume anapomzuia mkewe kuamua masuala
yake mwenyewe ambayo ni haki yake, kamwe mwanamke hawezi kuridhishwa na
hayo na hata kama ndoa imejaa watoto wazuri wenye afya na akili na fedha
nyingi zimeipamba nyumba yake.
Kama
mwanaume ataonyesha kutojali kuhusu matamanio au ndoto za mkewe kamwe
mwanaume huyo asitarajie kuwa mkewe atakuwa na upendo naye. Mwanamke
huwa anatamani sana kuona mumewe anajali na kuyapa uzito matamanio au
ndoto za mkewe. Kwa mfano mwanamke anapoonyesha kwamba, angependa
kuanzisha shughuli labda ya biashara au wangependa wapate mtoto na
mwanaume akaonyesha kutojali kuhusu matamanio hayo, kamwe mwanamke
hawezi kutulia na kuwa na amani.
Kuna
vitu au mambo ambayo mwanmke anayahitaji maishani, mahitaji hayo ni
mengi yakiwemo yale ya msingi katika maisha na yale ya kawaida. Inatosha
kusema kwamba, mwanamke anapogundua kwamba mumewe hajali juu ya
mahitaji yake huwa hajisikii vizuri.
Kwa
ujumla tunaweza kusema kwamba mwanamke huhitaji heshima katika utashi
na matamanio yake. Anapogundua kwamba utashi na matamanio yake
havizingatiwi na mumewe hawezi hata mara moja kumkubali mume huyo.
Kumkubali hapa ina maana ya kumkubali na kumtambua.
Hapo
ndipo tatizo ambalo ni la upande wa pili huanza. Kwa maumbile mwanaume
huwa anataka sana mkewe akimuonyesha kwamba anamthamini na kumtambua.
Labda hii inatokana na ubabe wa asili wa wanaume ambapo kila wakati
angependa kuona mwanamke akimgwaya na kuonyesha kwamba anamtambua kama
‘mwokozi’ wa aina fulani.
Kama
mwanamke anataka kumfanya mumewe amsikilize na kujali matamanio na
ndoto zake anachotakiwa kufanya ni kumuonyesha mumewe kwamba anamthamini
na kumtambua. Kwa mfano mwanaume anapofanya jambo ambalo hata kama
halina faida, lakini halina madhara, inabidi mkewe aonyeshe kuzitambua
juhudi hizo na kuonyesha kwamba, mume huyo anajitahidi sana katika
kufanya mambo yake.
Mwanaume
anahitaji sana kuona mwanamke akimsifu kwa juhudi anazofanya, iwe ni za
kitabia au za shughuli. Mwanaume anapokuwa na tabia nzuri, ni lazima
mwanamke atafute kila njia ya kumuonyesha kwamba ameitambua tabia yake
hiyo, kamwe asimuonyeshe kwamba juhudi anazofanya ni kupoteza muda. Pale
ambapo mwanaume huonyesha heshima kwa mkewe kwa kuzijali ndoto na
matamanio yake ya kimaisha, huhitaji sana kuonyeshwa kwamba heshima yake
hiyo imepokelewa. Kwa kawaida mume anapotimiza wajibu wake lazima mke
naye atimize wajibu wake.
Kuna
wakati na karibu mara zote, mwanamke huwa anamlaumu mwanaume na
mwanaume kumlaumu mwanamke kwa kila mmoja kudhani kwamba mwenzake ndio
chanzo cha matatizo. Hii ni kwa sababu wote wawili hawajui namna
nadharia hii inavyofanya kazi. Huyu anataka kuthaminiwa wakati hampi
mwenzake heshima na huyu anataka kupewa heshima wakati hamthamini
mwenzake.
Ili
kuondoa kulaumiana huko inabidi kila mmoja ajue wajibu wake, kwani kama
mmoja ataanza kumpa mwingine kile anachohitaji ni wazi huyu mwingine
atajibu kwa kumpa mwenzake kile kinachomstahili mwenzake ambacho ni
heshima
No comments:
Post a Comment