Wednesday 30 October 2013

Picha za mwili wa marehemu baba Wema Sepetu ulipoagwa jijini Dar jana jioni

BABA mzazi wa staa wa sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006/2007 Wema Sepetu, Balozi Abraham Isaac Sepetu ameagwa jana  jioni  nyumbani kwake Sinza - Mori jijini Dar es Salaam. 
 
Tukio hilo lilihudhuria na viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, Getrude Mongela pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe na wengine wengi waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu aliyefariki dunia Jumapili ya wiki iliyopita.
 
Waziri Membe kwa niaba ya serikali ametoa salamu za rambirambi na kuchangia kiasi cha shilingi milioni  1, “Kwa niaba ya serikali tumechangia kiasi cha shilingi milioni 1. Hata mimi pia nilimfahamu marehemu kwa muda mrefu na alikuwa kiongozi makini, Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi amen,” alisema Waziri Membe.
 
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa mazishi.
 
 
 
 
  
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment