Saturday, 9 November 2013

FAHAMU ADHARI ZA UTOAJI MIMBA

Utafiti mpya uliofanywa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii umeonyesha kuwa kutoboka kwa kibofu cha mkojo, kushamiri kwa kansa ya shingo ya uzazi, utasa na matatizo ya kisaikolojia kwa wanawake kunatokana na kasi kubwa ya utoaji mimba nchini. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Mtumwa Mwako(pichani), akizungumza mjini hapa jana, alisema ripoti ya utafiti huo inaonyesha kwamba, utoaji mimba ndiyo  chanzo kikuu cha matatizo mengi kwa wanawake.
 

Alisema licha ya mara nyingi utoaji mimba kufanywa na watu wenye utaalamu katika sekta ya afya wakiwamo wauguzi na waganga wanaokiuka maadili ya kazi zao, vitendo hivyo vinafanyika kwa usiri mkubwa.

“Kwa mujibu wa tafiti hiyo, wakati wa utoaji mimba kuna uwezekano mfuko wa uzazi kutobolewa, vipande vya mwili wa mtoto anayetolewa  kubaki tumboni kutokana na haraka na kukosa ujuzi, hali ambayo yaweza sababisha  mauti kutokana na kutokwa kwa damu nyingi wakati wakitendo hicho” alisema Dk. Mwako.

Alisema pia mtoaji mimba anaweza kushindwa kubeba mimba  nyingine kutokana na mimba  hizo kutunga nje ya kizazi na  kuharibika muda mfupi baada ya kupata ujauzito.

Aliwataka vujana wa kike kuacha tabia ya kutoa mimba kwani kunahatari kubwa kwa afya zao, huku akiisisitiza jamii kuwaelimisha vijana madhara ya utoaji mimba ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo limeshamiri katika sehemu nyingi nchini hasa mijini. 


“Jamii yote ishirikiane na wataalamu wa afya katika kutoa elimu kwa vijana kuepuka tabia ya utoaji mimba ili kuokoa taifa” alisema Dk. Mwako.

No comments:

Post a Comment