Monday 4 November 2013

KATIKA SAFU YA UREMBO LEO:Urembo wa Midomo/ Lips

Midomo ni sehemu muhimu sana katika kukamilisha unadhifu wako. Inaweza ikakufanya uonekane una mvuto zaidi na kuongeza kupendeza katika muonekano wako.
Ngozi ya midomo ni laini sana na inahitaji uangalizi wa hali ya juu kuhakikisha inakuwa ni laini siku zote.
Kuna wapenzi wa mafuta ya kawaida/mgando/vaseline, lipstic, lipshine na wengine si watumiaji kabisa wa chochote.

Ngozi ya midomo inahitaji kuwa exfoliated/kutolewa ngozi ngumu ya juu iliyokufa unaweza kutumia mswaki wako baada ya kupiga mswaki pitisha kwa uangalifu kwenye midomo yako kisha paka vaseline/mafuta ya mgando/lipshine/lipstic. Ni vizuri zoezi hili likafanyika usiku wakati ukijiandaa kulala itakufanya ukiamka uwe na lips zilizo laini na zenye mvuto zaidi.Kunywa maji mengi ya kutosha ili kufanya ngozi ya mwili wako na ya midomo kuwa laini na nyororo.

Matumizi ya lipstick/lipshine ni muhimu kuzingatia siku ya mwisho ya matumizi yake (use by date) hii ni kuhakikisha hujiweki kwenye hatari ya kuharibu midomo yako badala ya kuiremba.

Upakaji wa lipstick
1. Tumia brush ya lipstick kupaka lipstick yako hii itasaidia kutumia kiasi kidogo.


2. Ikutanishe midomo yako baada ya kupaka lipstick hii itasaidia kuifanya idumu muda mrefu zaidi ondoa kwa kitambaa laini/tissue iliyozidi.

3.Paka kwa mbali lipgloss ili kung'arisha midomo yako ila waweza kuiacha lipstick peke yake kama hupendelei lipgloss au midomo yako kung'aa.

Jirembe mwanadada.....na jiangalie mvuto wako.....

No comments:

Post a Comment