UKIFUATA MAMBO HAYA KUMI UTAKUA UMERAMBA SUMU YA PENZI NA HAUTOUMIZA/HUTOUMIZWA KAMWE…
1. Wivu Wa Kupindukia
Ni
Jambo Jema Kwa Mwanamume Kumtakia Heri Mpenzi Wake Na Kufanya Kila
Awezalo Kuhakikisha Kuwa Hapati Madhara, Lakini Iwapo Utakuwa Mtu Wa
Wasiwasi Na Mashaka Pale Unapomwona Mpenzi Wako Akizungumza Na Mwanamume
Mwingine, Au Anapotoka Na Marafiki Zake Wa Kike, Au Anapovaa Nguo
Inayomfanya Atamanishe, Basi Fahamu Kuwa Tayari Umekunywa Sumu Ya
Mapenzi.
Katika Uhusiano Wa Kimapenzi, Kuaminiana Ni Jambo
Muhimu Sana. Kama Kweli Unataka Mpenzi Wako Akupende Kwa Dhati, Mwoneshe
Kuwa Unamwamini Na Unaheshimu Maamuzi Yake, Ikiwa Ni Pamoja Na Maamuzi
Ya Kutoka Na Marafiki Zake Wa Kike Na Kuwa Na Marafiki Wa Kawaida Wa
Kiume. Ondoa Hofu Na Acha Kabisa Kumpeleleza, Maana Wapo Wanaume Ambao
Hutumia Muda Wao Mwingi Kuwapeleleza Wapenzi Wao Ikiwa Ni Pamoja Na
Kuwategeshea Kamera Na Rekoda Za Simu.
2. Kutomwachia Nafasi Mpenzi
Kama
Huishi Na Mpenzi Wako Ni Jambo La Kawaida Kuwa Na Hamu Ya Kumwona Mara
Kwa Mara, Lakini Kumbuka Kuwa Mpenzi Wako Naye Ana Maisha Yake Na
Anahitaji Nafasi Ya Kuwa Peke Yake Kwa Ajili Ya Mambo Yake Binafsi.
Hisia
Za Kutaka Kuwa Na Mpenzi Wako Muda Wote Zinaweza Kudhaniwa Kuwa Ni Za
Mapenzi Ya Dhati, Lakini Kwa Hakika Hiyo Si Ishara Njema Ya Mapenzi Ya
Kudumu. Hebu Jiulize Kama Unaweza Kuendeleza Hali Hiyo Maisha Yako
Yote. Ni Wazi Kuwa Utachoka. Kwa Hiyo, Mpe Mpenzi Wako Fursa Ya
Kupumua. Namna Hii Mpenzi Wako Atajenga Hamu Ya Kutaka Kukutana Nawe
Lakini Ukiwa Naye Muda Wote Hamu Hiyo Itaisha.
3. Kumwamulia Mpenzi Mambo Yake
Unaweza
Kujikuta Ukisukumwa Kumwambia Mpenzi Wako Awe Anavaa Nini Wakati Gani,
Akutane Na Nani Na Kwa Wakati Gani Au Ale Nini. Ukiona Hivyo, Fahamu
Kuwa Hayo Si Mapenzi, Bali Umepitiliza Na Pengine Mwisho Wa Uhusiano
Wenu Unanukia.
Hata Ukiachilia Mbali Suala Zima La Usawa Wa
Jinsia, Hakuna Mwanamke Ambaye Angependa Apangiwe Kila Kitu Kuhusiana
Na Maisha Yake. Kama Ilivyodokezwa Hapo Juu, Kila Mtu Ana Maisha Yake
Na Kilichowaunganisha Ni Mapenzi Tu. Kama Utataka Kumpangia Kila Kitu
Ni Wazi Kuwa Utaishia Kuishi Peke Yako.
4. Kumuuliza Mpenzi Maswali
Iwapo
Utajikuta Ukimuuliza Mpenzi Wako Maswali Mengi Yanayoonesha Wasiwasi
Wako Kuhusiana Na Mwenendo Wake, Fahamu Kuwa Kuna Tatizo Na Tatizo Hilo
Lisipopatiwa Ufumbuzi Utakuwa Mwanzo Wa Mwisho Wa Uhusiano Wenu.
Mwanamke
Angependa Umuulize Maswali Ya Kawaida Kuhusiana Na Jinsi Siku Yake
Ilivyokuwa Na Kama Marafiki Zake Hawajambo Au La, Lakini Kila Jambo
Lina Mpaka Wake. Mwanamke Hatarajii Kuwa Kila Mnapokutana Atakuwa Kama
Ameingia Kwenye Chumba Cha Mtihani Au Usaili Wa Kazi.
5. Kutoamini Anachokweleza Mpenzi
Wakati
Mwingine Watu Hushindwa Kuwaamini Wenzao, Lakini Kwa Sababu Ambazo Ni
Za Msingi, Lakini Kuna Wakati Ambapo Mtu Hushindwa Kumwamini Mwenzake
Bila Sababu Yoyote Ya Msingi, Au Kwa Sababu Zisizo Sahihi, Kisingizio
Kikiwa Ni Mapenzi.
Kuna Tatizo La Kisaikolojia La Kujishuku Au
Kuwashuku Wenzako. Hili Ni Jambo Ambalo Linaweza Kukuharibia Mustakabali
Wako Katika Mapenzi, Maana Husababisha Kujengeka Kwa Mazingira Ya
Kutokuaminiana. Ili Uweze Kwenda Sanjari Na Mpenzi Wako, Amini Kila
Anachokweleza Hadi Pale Utakapokuwa Na Sababu Za Msingi Za
Kutokumwamini. Na Hata Unapokuwa Umelithibitisha Jambo, Endelea Kuwa
Katika Uhalisia Wako.
6. Kuacha Hobi, Marafiki
Mahusiano Ya
Kimapenzi Mara Nyingi Huhusisha Kila Mmoja Kuacha Baadhi Ya Mambo Yake
Kwa Ajili Ya Mwenzake. Hata Hivyo, Lengo Ni Kuweka Tu Uwiano Wa
Mahitaji, Si Kuacha Kila Kitu Ulichokuwa Nacho Kwa Ajili Ya Mwenzako,
Ama Kwa Shinikizo, Au Kwa Kulewa Penzi.
Iwapo Utabaini Kuwa
Marafiki Zako Sasa Wamekuwa Ni Marafiki Zako Wa Zamani Na Hobi Zako
Zimebaki Tu Katika Kumbukumbu Japo Kwa Hakika Bado Unahisi Mapenzi
Katika Hobi Hizo, Basi Tambua Kuwa Huyo Mrembo Wako Amekunywesha Sumu
Ya Penzi Na Sasa Huwezi Hata Kuitumia Vema Mantiki Yako.
Mbaya
Zaidi, Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki Zako Wapya Ni Marafiki Wa Siku Zote
Wa Mpenzi Wako Na Hobi Zako Ni Zile Za Mpenzi Wako, Basi Tambua Kuwa
Huna Tena Nafsi Yako, Bali Umejisalimisha Mzima Mzima Kwa Mpenzi Wako.
Lakini Msemo Mmoja Wa Hekima Unatwambia Usiweke Mayai Yako Yote Kwenye
Kikapu Kimoja. Yamkini Unaelewa.
7. Kukubali Kupelekeshwa
Pengine
Unakumbuka Kuwa Kuna Nyakati Ambapo Ulikuwa Na Uwezo Wa Kujikita
Katika Jambo Moja Na Kulifanya Kwa Umakini, Huku Ukiwa Pia Mwerevu,
Mjanja Na Unayejisimamia, Lakini Leo Unayeyuka Kirahisi Tu Kama Barafu
Iliyowekwa Juani! Hii Ni Hatari Kwa Mustakabali Wa Maisha Yako.
Mbaya
Zaidi Ni Pale Utakapoiacha Kazi Yako Inayokulipa Vizuri Na Kufanya
Kazi Nyingine Kwa Ajili Ya Kumfurahisha Mpenzi Wako. Ukifika Hali Hii
Ujue Wewe Mwenyewe Kuwa Hapo Hakuna Mwanamume.
8. Utayari Wa Kufa Kwa Ajili Yake
Umewahi
Kujisikia Kuwa Na Utayari Wa Kufa Kwa Ajili Ya Mpenzi Wako? Kama Jibu
Ni “Ndiyo”, Basi Fahamu Kwa Hakika Kuwa Hayo Uliyo Nayo Si Mapenzi Bali
Ni Upumbavu. Pengine Huku Ndiko Kunywesha Sumu Ya Mapenzi. Kwa Hakika,
Hakuna Mwanamke Ambaye Anastahili Kumfanya Mwanamume Yeyote Kufa Kwa
Ajili Yake.
Yamkini Wanaume Wanaolengwa Katika Makala Haya Si
Wavulana Wanaosoma Sekondari, Waliobalehe Majuzi, Ambao Wakipenda Au
Kupendwa Hujiona Kama Wako Katika Sayari Yao. Mwanamume Aliyepevuka
Hujiamini Na Hayaweki Maisha Yake Yote Mikononi Mwa Mwanamke, Hata Kama
Mwanamke Huyo Angekuwa Ndiye Mrembo Wa Dunia.
Iwapo, Ama Kwa
Ujinga Au Kwa Kufahamu Umewahi Kumwambia Mpenzi Wako: “Ukiniacha
Nitajiua,” Na Ukawa Unaamini Hivyo Kabisa, Basi Yamkini Unahitaji
Kutafuta Msaada Wa Ushauri Nasaha, Maana Kwa Hakika Umepotoka.
9. Muda Wote Unawasiliana Naye
Vijana
Wa Siku Hizi Ni Watumiaji Wazuri Sana Wa Simu, Lakini Iwapo Utabaini
Kuwa Asilimia Kubwa Ya Muda Wako Unautumia Ama Kwa Kuongea Au
Kuwasiliana Kwa Ujumbe Mfupi Na Mpenzi Wako, Basi Fahamu Kuwa Kuna
Tatizo Ambalo Linahitaji Ufumbuzi Wa Haraka.
Kumbuka Kuwa
Mapenzi Hayachukui Nafasi Ya Kila Kitu. Yamkini Huyo Mpenzi Wako
Amekukuta Unaishi Na Kuna Mambo Ya Muhimu Ya Kufanya. Hebu Achana Na
Simu Kwanza Ufanye Mambo Ya Muhimu Kuhusiana Na Maisha Yako. Kama Mpenzi
Wako Hakwelewi Katika Hili Basi Hakufai.
10. Ndugu Zake Wanakufuatilia
Iwapo
Utabaini Kuwa Marafiki, Ndugu Na Jamaa Za Mpenzi Wako Wanamtonya
Mpenzi Wako Kuhusiana Na Kile Wanachokiita Mwenendo Wako Mbaya, Usipuuze
Hali Hii. Kuna Uwezekano Mkubwa Kuwa Watu Hawa Wanayo Sababu Ya Kuwa
Na Wasiwasi Na Mwenendo Wako, Kwa Hiyo Jichunguze Na Kuangalia Jinsi
Unavyoenenda.
Hata Hivyo, Jambo Hili Si Ishara Njema Ya
Mustakabali Mwema Wa Uhusiano Wenu. Iwapo Mpenzi Wako Ataweka Watu Wake
Wakufuatilie, Maana Yake Halisi Ni Kwamba Hakuamini. Katika Hali Kama
Hii, Haitarajiwi Kuwa Mustakabali Wa Uhusiano Wenu Utakuwa Mzuri, Kwani
Kutakuwa Na Uingilizi Mwingi Wa Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zake. Unaweza
Kukubali Kuendelea Kuishi Katika Hali Hii Kwa Kisingizio Cha Mapenzi,
Lakini Ukweli Ni Kwamba Hayatakuwa Mapenzi Bali Karaha.
KUWA MAKINI
Kama
Unavyoona, Hizi Ni Baadhi Tu Ya Dalili Kuwa Mapenzi Yako Kwa Mwanamke
Sasa Yanaelekea Katika Ulevi, Mithili Ya Ule Wa Dawa Za Kulevya. Jambo
Moja La Kukumbuka Ni Kwamba Kweli Mapenzi Ni Kitu Kizuri, Lakini Pia
Mapenzi Yanahitaji Kuwa Jambo Linaloashiria Mustakabali Mwema Kwa
Wahusika Wawili. Yakiwapo Mambo Haya Kumi Hauwezi Kuwapo Mustakabali
Mwema Katika Mapenzi.
No comments:
Post a Comment