Simba imefikia uamuzi huo baada ya mapendekezo ya kocha wao
mpya, Mcroatia Zdravok Logarusic, ambaye aliambia Mwanaspoti kuwa
ameutaka uongozi usajili kipa, beki wa kati na ikiwezekana mshambuliaji.
Mwanaspoti ilizungumza kwa simu na Musoti
aliyejiunga na Gor Mahia mwaka 2011 akitokea Nairobi City ambaye
alisema: “Ni kweli tumezungumza, lakini bado sijasaini nafikiri muda
wowote mambo yakienda sawa tutamalizana, kwa sasa nawasubiri wao tu.”
Musoti ambaye alikuwa akiendesha gari wakati
anazungumza na Mwanaspoti, alimpa simu mkewe, Lilian kwa ajili ya
ufafanuzi zaidi: “Ongea na huyu (mkewe),” alisema Musoti.
Naye, Lilian alisema: “Iko hivi, bado hajasaini, makubaliano tayari na tunawasubiri wenyewe kwa ajili ya kumalizana kabisa.”
“Tunataka mambo yakamilike kabisa na ndiyo
tutaweza kuzungumza kwa undani zaidi, si unajua huyu alikuwa na Gor
Mahia,”alifafanua, Lilian.
Kuhusu Ivo ambaye yupo nchini Kenya na kikosi cha
Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya Chalenji yeye alizungumza na gazeti
hili jana mchana na alisema: “Niliambiwa leo hii (jana) kuwa
ningesaini, lakini hadi sasa bado sijawaona, naendelea kusubiri na
nafikiri muda wowote mambo yanaweza kwenda kama tulivyokubaliana.”
Mbali na kuzungumza na kipa huyo, Mwanaspoti pia
lilikutana na Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala jana usiku jijini
Nairobi ambaye licha ya taarifa ambazo Mwanaspoti ilizipata lakini
aligoma kuzungumzia usajili huo.
Awali, Logarusic alisema kuwa amechagua wachezaji
kutoka Kenya kwa sababu anawajua baada ya kufanya nao kazi alipokuwa
anaifundisha Gor Mahia.
Logarusic alisema: “Nahitaji wachezaji watatu kwa
nafasi ya kipa, beki wa kati na kama kutakuwa na ulazima sana, asajiliwe
pia mshambuliaji.
“Kati ya wachezaji hao, Ivo ni mmoja wao na mimi
ndiye nimependekeza asajiliwe ingawa kulikuwa na makipa wengine zaidi
kama kumsajili yeye itashindikana.”
Alipoulizwa mapungufu ameyajuaje wakati Simba ina
mshambuliaji, Tambwe Amissi na beki wa kati Gilbert Kaze, kutoka Burundi
na beki wa kati, Joseph Owino kutoka Uganda, Logarusic alisema: “Ni
kweli bado sijawaona na ndiyo maana nasisitiza nahitaji kuwaona na
kuwafahamu zaidi. Mapendekezo yangu ni kwa sababu ya kuhakikisha Simba
inafanikiwa.”
Katika kikosi cha Gor Mahia, Musoti hucheza
sambamba na Ivan Anguyo au Edwin Lavatsa wakati golini hucheza kati ya
Jerim Onyango au Ivo Mapunda akiwa Simba huenda akashirikiana na kati ya
Owino au Kaze au hata Hassan Hatibu anayeibukia katika safu ya ulinzi
wa kati..
.
No comments:
Post a Comment