Friday, 13 December 2013

Viwanja 12 vitakavyotumika fainali kombe la dunia 2014



 Lakini, uwanja huo wa kihistoria ni moja ya viwanja 12 katika miji 12 tofauti itakayotumika kwa ajili ya fainali hizo za soka zitakazoshuhudia timu 32 zikimsaka mwamba mmoja wa Dunia.
MECHI ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil itapigwa kwenye Uwanja wa Maracana, Julai 13, 2014.
Lakini, uwanja huo wa kihistoria ni moja ya viwanja 12 katika miji 12 tofauti itakayotumika kwa ajili ya fainali hizo za soka zitakazoshuhudia timu 32 zikimsaka mwamba mmoja wa Dunia.
Makala hii inazungumzia viwanja vyote 12 vitakavyotumika kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia ambazo zitaanza rasmi Juni 12 mwakani kwa mechi ya Brazil dhidi ya Croatia itakayopigwa kwenye Uwanja wa Arena Corinthians jijini Sao Paulo.
Uwanja: Maracana
Jiji: Rio de Janeiro
Uwezo: Watazamaji 73,531
Klabu zinazoutumia: Fluminense FC na CR Flamengo
Rio de Janeiro ni jiji la aina yake Brazil na hakika Uwanja wa Maracana una historia ya kipekee katika soka la Dunia. Maracana ilijengwa upya kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia mwakani. Ulifunguliwa Juni mwaka huu kwa mechi ya kirafiki kati ya Brazil na England.
Ndiyo uwanja utakaotumika kwa fainali Julai 13 mwakani, mandhari yake nzuri ndicho kitu kinachovutia zaidi kwenye mji huo kutokana na kuwa na fukwe safi na vivutio vingine vya kitalii kama Mlima wa Sugar Loaf na Sanamu ya Christ the Redeemer.
Maracana ulitumiwa kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 1930, ambapo mashabiki 200,000 waliingia na kuishuhudia Uruguay ikiichapa Brazil
Mechi zitakazochezwa:
Juni 15, 2014 - Argentina v Bosnia&Herzegovina - Kundi F

No comments:

Post a Comment