ROSE Ndauka ambaye ni mama anayetamba kwenye filamu za Bongo,
amewaonya wasanii wa kike kuachana na biashara ya utoaji mimba kwani ni
kinyume cha maadili na kujidhalilisha.
Alisema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu nyota hawataki kuzaa
hata wale waliozaa kabla ya kuwa nyota hawapendi kujulikana kama
wamezaa, kitu ambacho hakina maana katika maisha ya msanii bali ni
kujichelewesha tu.
“Mimi sijui ni kwa nini baadhi ya mastaa hawataki kuzaa, ni
suala la kujipanga tu, kama una kipaji kipo tu hakiwezi kupotea sababu
eti ya kuzaa,” alisema Rose na kuongeza kuwa kadri umri unavyokwenda na
fursa ya kuzaa inapotea na wengi hawajui umuhimu wa kuzaa mapema.
Ingawa anasema kuna woga wa majukumu ya kulea kwa baadhi ya
vijana wa kisasa na si wasanii peke yao. Rose hivi karibuni alijifungua
mtoto wa kike na kumpa jina la Naveen.
No comments:
Post a Comment