Friday, 24 January 2014

HATA KAMA UMZURI, BILA UTUNDU FARAGHA HUNA NYIMBO!


 Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati.


Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.


Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanaranda mtaani.


Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa kipekee kwake.


Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu na ubunifu katika uwanja wetu ulee wa kujidai.


Faragha ni eneo muhimu sana ambalo linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote yaani mke na mume.


Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe kwa kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha iliyokamilika.
Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa kirefu wanawake. Kuna wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji. 


Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati kubwa kwani kwa hali ilivyo sasa, wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.


Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa lakini wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.
Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake wengi walio ndani ya ndoa licha ya uzuri walionao, siku hizi wanasalitiwa sana.
Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji mno lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao.


Hawajui kitu, wamekaa kama magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa na ndoa zao zitadumu, zitadumu kwa misingi ipi?
Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje.


Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa, ipo siku utajikuta ni mke wa pambo la nyumba tu.
Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo, wanaume walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia. 


Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo zinazoonekana kuwashika waume za watu siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.


Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya ndoa usifanye yale wanayofanya nyumba ndogo? Je, uko tayari kuachika eti kwa kuwa huoneshi kuwa mzoefu pale faragha unapokutana na mzee?
Hata kama si mjuaji kwenye mambo mengine lakini unatakiwa kujifunza. Waulize watu wenye uzoefu, najua watakufundisha yapi ya kufanya ili kumshika mumeo. Kinyume chake ni kwamba, hata kama umzuri kiasi gani mumeo atakusaliti na unaweza kujikuta unatoswa kabisa.



No comments:

Post a Comment