Jumapili iliyopita, wakati Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, akitangaza mabadiliko ya nafasi za mawaziri na manaibu wao kama Rais Jakaya Kikwete alivyoteua, Magufuli alikuwa ‘bize’ akikagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Kutokana na kitendo hicho, baadhi ya waliomshuhudia walisema: “Huyu ndiye kamanda, aisee ni noma sana!”
Kauli hiyo, ilitokana na ukweli kwamba Magufuli hakuwa na wasiwasi wala mchecheto kuhusu nafasi za mawaziri na kuonesha kwamba anajiamini na yupo kikazi zaidi, ndiyo maana aliamua kuzipa kisogo taarifa kutoka ikulu na badala yake kusimamia ujenzi wa daraja hilo ambalo linatajwa kuwa la kihistoria.
“Muda ambao Magufuli alikuwa anakagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni, mawaziri na manaibu wengi walikuwa wakifuatilia taarifa ya Balozi Sefue kwenye vyombo vya habari kuhusu mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete.
“Magufuli hakujali kabisa hilo, ndiyo maana alichokifanya ni kwenda kukagua daraja hilo ambalo likikamilika, litaacha heshima kubwa kwa Rais Kikwete,” alisema Mwisege Kimbati katika maoni kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Rebecca Mwizarubi katika maoni yake Facebook, alisema: “Ni Jumapili, ni wikiendi, watu wapo kwenye mapumziko, wengine wanastarehe kama siyo na familia basi katika viwanja mbalimbali lakini Magufuli yupo kazini anachapa kazi. Tunahitaji viongozi wa aina yake. Magufuli ni hazina ya nchi hii.”
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mitandao mingi ‘iliposti’ picha hizo za Magufuli na wachangiaji wake walimsifu Magufuli kwa kupiga kazi bila kujali kwamba ilikuwa Jumapili, vilevile kwa kutokuwa na wasiwasi kuhusiana na taarifa ya mabadiliko ya mawaziri.
No comments:
Post a Comment