Wednesday, 22 January 2014

Mata asajiliwa na Manchester United

Ombi la Manchster United la kutaka kumsajili nyota wa Chelsea Juan Matata imekubalika.
Ripoti zinasema United imetumia takriban kitita cha pauni milioni 37 kumsajili mcheza kiungo huyo wa Chelsea.

 
Juan Mata
 
Mata mwenye umri wa miaka 25, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu baadaye hii leo, kabla ya kukamilisha usajili huo.

Mchezaji huyo kutoka Uhispania anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu hiyo iliyo na makao yake katika uwanja wa Old Trafford.

Mata ambaye aliichezea Chelsea, mechi 32, aliwaaga wachezaji wenzake na wakufunzi wa Chelsea katika uwanja wao wa mazoezi wa Cobham siku ya Jumatano.

Manchester United yakana fununu

Kocha wa Manchester United David Moyes

Awali kulikuwa na fununu kuwa Mata mwenye umri wa miaka ishirini na mitano, alitaka kuondoka kutoka Chelsea, baada ya kushinda kupata nafasi miongoni mwa wachezaji wa kwanza kumi na mmoja wa Chelsea, chini ya kocha wao mpya Jose Mourinho.
Siku ya Jumanne, Chelsea ilitangaza kuwa hawana nia yoyote ya kumuuza nyota wake Mata, ambaye aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa klabu hiyo mwaka uliopita.

Lakini mchezaji huyo ambaye alikuwa kikosi cha Uhispania kilichoshinda kombe la dunia mwaka wa 2012, aliondolewa katika mechi tisa kati ya kumi na tatu alizocheza za ligi kuu ya premier msimu huu, hali iliyozua fununu kuwa huenda akauzwa mwezi huu wa Januari.

Kwingineko klabu ya Cardif inatarajia kumsaini mchezaji wa Manchester United Wilfred Saha kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Zaha mwenye umri wa miaka ishirini na moja alifanyiwa uchunguzi wa matibabu siku ya Jumatano na Cardiff inataka kukamilisha usajili huo kabla ya mechi yao ya raundi ya nne ya kuwania kombe la FA dhidi ya Bolton.

No comments:

Post a Comment