Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja (jina tunalo) mkaazi wa Junguni Gando aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Wete akipatiwa matibabu baada ya kupigwa na baba yake mzazi kutokana na utofauti wa sura zao, amefariki dunia siku ya Jumatano alfajiri saa10.30 .
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Daktari
wa Wodi ya Watoto wa hospitali hiyo, Sada Juma Mbwana zinasema, mtoto
huyo amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata.
“Mtoto alipofikishwa hospitalini tuliambiwa kwamba
anasumbuliwa na kifua (anakohoa) lakini mambo yalikuwa mengine baada ya
Polisi kufika wakiwa na PF3 na ndipo mama mzazi alipoeleza mwanawe
amepigwa na baba yake,” alifahamisha Sada
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba,Shakhan
Mohammed Shakhan amesema baba mzazi wa mtoto huyo anashikiliwa kutokana
na tuhuma za kujeruhi,anatarajia kufikishwa mahakamini Jumatatu ijayo.
No comments:
Post a Comment