Rais Kikwete anatakiwa kufuta alichokizungumza ndani ya siku tatu.” Benson Kigaila
Kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni ndogo na kutokana na vitendo vinavyofanywa na viongozi na wanachama wa Chadema kuvuruga amani nchini,” alisema na kuongeza kuwa dawa ya moto ni moto.
Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta kauli yake ya kuwataka wana CCM kuacha unyonge na kujibu mapigo dhidi ya upinzani na ametakiwa kuomba radhi ndani ya siku tatu, vinginevyo suala hilo litafikishwa jumuiya za kimataifa.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga
Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki
iliyopita, ambapo Chadema wanaitafsiri kama kielelezo cha kuvuruga
amani ndani ya nchi.
Kwa majibu CCM kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kamwe hawatafanya hivyo.
“Kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni ndogo na kutokana
na vitendo vinavyofanywa na viongozi na wanachama wa Chadema kuvuruga
amani nchini,” alisema na kuongeza kuwa dawa ya moto ni moto.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema,
Benson Kigaila alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kufuta
alichokizungumza ndani ya siku tatu kuanzia jana, vinginevyo
watalifikisha suala hilo mbele ya jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya
malalamiko yao.
Alisema kuwa Rais Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu, na
alihoji kwanini awatake WanaCCM kujibu mapigo dhidi ya wapinzani badala
ya kuacha hatua za kisheria zikafuatwa kwa kutumia vyombo husika ambavyo
ni polisi na majeshi na mahakama.
No comments:
Post a Comment