Jana February 25 Uongozi wa hospitali ya taifa muhimbili kwa kushirikiana na
maafisa wake wa usalama wamemnasa daktari feki aliyekuwa akiwatapeli
fedha wagonjwa na watu mbalimbali wanaofika kwa ajili ya kupatiwa huduma
za matibabu katika hospitali hiyo.
Taarifa kutoka Muhimbili inasema ni Tukio la tatu kutokea katika
hospitali hiyo ingawa matukio ya namna hiyo yameshawahi kuripotiwa
katika baadhi ya hospitali kubwa za serikali kwa baadhi ya watu
wanaotumia mwavuli wa fani ya udaktari kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu.
Msemaji wa Hospital ya taifa Muhimbili Aminieli Aligaesha amemtaja
Daktari huyo feki kwa jina la Kitano Mustapha na kubainisha kuwa katika
upekuzi uliofanywa na maofisa usalama wa hospitali hiyo wamemkuta
mtuhumiwa akiwa na kadi tatu za kliniki,namba za simu za madaktari na
wauguzi katika hospitali hiyo huku wakitambua kufanya hivyo ni kosa kwa
mujibu wa sheria zilizopo na kanuni za utabibu.
Daktari huyo feki Kitano Mustapha amekana kutohusika na utaperi huo
kwa wagonjwa mbali mbali wanaofika kupata huduma za kimatibabu na kusema
hawezi kuongea lolote mpaka Mwanasheria wake awepo.
No comments:
Post a Comment