Wednesday, 22 May 2013

Mapigano Mtwara watu watatu wauawa.......


Hivi ndivyo hali ilivyokuwa Mtwara miezi minne iliyopita,leo hali imekuwa mbaya zaidi ya kipindi hicho.


WATU watatu wamefariki Dunia katika mapambano ya Askari Polisi na Wananchi waliokuwa wakiandamana kupinga hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyosomwa leo na Waziri Profesa Sospeter Muhongo.
Mbali na watu hao kuuawa Askari mmoja wa Jeshi la Polisi pia amejeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa mshare katika mapambano hayo yaliyoanza saa 12 asubuhi,katika maaeneo mbalimbali yaliyokuwa yametekwa na waandamanaji hao.
Waandishi wa habari  waliokuwa katika maeneo ya Mikindani anaripoti kwamba watu hao waliuawa katika eneo hilo baada ya kutokea kwa mapambano makali kati ya waandamanaji na Askari Polisi.
Mbali na mauaji hayo pia kumetokea uharibifu mkubwa wa mali katika eneo hilo ambapo ofisi  za serikali zimevamiwa na kuchomwa moto huku daraja la Mikindani nalo likivamiwa na kuvunjwa ili kuzuia mawasiliano pamoja mwingiliano wa watu kutoka Mtwara mjini kuingia eneo hilo.
"Mapambano ni makali katika eneo la Shangani huku waandamanaji hao wakielekea kwenye nyumba za vigogo zilizopo jirani na eneo mapigano kwa sasa, hivi tunavyozungumza tumehifadhiwa katika Kanisa moja hapa maeneo ya sokoni, na kuna nyumba moja ya kulala wageni (Shengena Lodge) pia imechomwa moto kwa madai kwamba iliwalaza Askari Polisi walioingia hapa Mtwara tangu juzi kwa ajili ya kuthibiti machafuko, hali ni mbaya milio ya risasi na mabomu ndiyo yanayosikika"alisema mwandishi wetu.

No comments:

Post a Comment