SIJUI
wewe ulikuwa una malengo gani wakati unafikiria kuwa na ambaye unaye;
wapo ambao walikuwa na malengo kwamba akiwa na mwanaume, maana yake awe
ndio sawa na mashine ya kutolewa fedha maarufu kama ATM.
Ikiwa
ulichokuwa unatafuta ni mwanaume au mwanamke ambaye kwako atakuwa ni
ATM, kwamba ndiye awe anakupa kila kitu unachotaka, ikiwa hatakuwa na
fedha si rahisi mkaendelea kuwa na uhusiano mzuri, kwa kuwa mpango wako
haukuwa mapenzi, bali kuchuma fedha na kula raha.
Wajinga
ni wale ambao wanaingia kwenye mapenzi ili kusaidiwa tu, badala ya
kusaidiana. Mwenye hekima ni yule ambaye anafahamu kwamba kuingia kwenye
mapenzi, maana yake ni kuongeza timu ya kusaidiana katika maisha, si
vinginevyo.
Mwanamke
yeyote ambaye anafikiri yuko na mwanaume maana yake ni kwamba awe
anamnunulia kila kitu, kwamba kwake mwanaume ni kila kitu, kinywaji
anunuliwe, chips anunuliwe nk...kwamba yeye ni mtu wa kupewa tu ofa,
maana yake ni kwamba akili yake imekufa.
Kufikiri
kwamba kuoana na fulani maana yake ni sasa yeye atakuwa anakusaidia
kila kitu milele na kwamba asipofanya hivyo utamdharau, si kitu sahihi.
USIWE NA MATARAJIO MAKUBWA UNAPOINGIA KWENYE NDOA
Unapoingia
kwenye ndoa, usiwe na matarajio makubwa sana mazuri. Jambo unalopaswa
kufahamu ni kuwa uhusiano ni suala la kawaida, kwamba unakuwa na mtu kwa
lengo la kuwa nae kama timu moja kusaidiana katika kuleta maendeleo.
Kati
ya mambo yanayofanya watu kutofurahia mapenzi, ni pale anapotishwa
kwamba labda asipofanya hiki kwa mfano kukusaidia, basi uhusiano wenu
utaharibika.
Kuna
wanawake utasikia aaah sasa kuna maana gani ya kuwa na mwanaume ikiwa
namwomba fedha hawezi kunisaidia? Fikra kama hii ni ya kipuuzi. Wewe
kwanini huna fedha? Ndoa ni kusaidiana, sio kugeuzana ATM.
YUKO BIZE NA SIMU, KOMPYUTA NK
Kati
ya mambo yenye kutiana ‘kichefuchefu’ katika mapenzi ni pale kwamba uko
na mwenzi wako, lakini ni kama wewe ni tambala la deki; yaani yuko bize
na simu yake au kompyuta au kitu kingine chochote.
Wengine
unakuta labda anawasiliana na wengine kwa mitandao ya kijamii kama vile
facebook, twitter nk, kumaanisha kwamba wewe ni muhimu, walio muhimu ni
wale ambao anawasiliana nao huko.
KUKOSOANA MBELE ZA WATU AU HATA KUPIGANA
Wapo
watu wamekuwa na tabia ya kukosoana au hata kupigana mbele za watu.
Kati ya makosa yenye kukera na huenda ukasababisha uhusiano ukabaki
historia ni hii...ni vizuri ndugu yangu kujifunza namna ya kuachana na
hasira kali.
MATUMIZI MABAYA YA FEDHA NA KUTOKUWA NA MIKAKATI KATIKA MAISHA
Kila
mtu Duniani anataka maisha bora, kwa maana hiyo ni furaha ya kila mtu
kuona mwenzi wake anakuwa mwenye mikakati imara katika kuimarisha maisha
yao.
No comments:
Post a Comment