Wednesday, 19 February 2014

Mambo 16 ya msingi ambayo kama upo kwenye uhusiano au unatarajia kuwa na uhusiano na binti au kijana wa kiume unatakiwa kuyazingatia kikamilifu

1. Huwezi kuwapenda watu wa nje kama huna mapenzi ya dhati kwayule uliyenaye kwenye uhusiano sasa.


2. Kumsaliti mwezio kwa kisingizio cha kulipiza kisasi huwa njia rahisi ya kukuingiza katika mgogoro binafsi na mwishowe kukuharibia kila mipango yako

3. Kamwe usijidanganye kuwa utaweza kumsaliti na kumdanganya mwenzio kwa muda murefu bila kugundulika, kila usaliti ni sawa na mimba lazima kuna muda utafika kila mtu ataiona tu

4. Mahusiano yoyote hujengwa na uaminifu na kuthaminiana huku neon samahini na nimekusamehe likiwa nguzo kwa utatuzi wa kila tatizo mbele yenu

5. Kusema nisamehe sio kuonekana mjinga bali pia huweza kukupa heshima na kuongeza mapenzi ya dhati baina ya yenu

6. Neno nitakuacha au tuachane isiwe silaha ya kumwonea mwenzio maana nalo likizoeleka huweza kumfanya mwenza wako kuchukua maamuzi magumu kwani
huashiria wewe una watu huko nje wakupao kiburi

7. Kamwe usiwe mwepesi wa kuamini nini watu wanasema ila mshirikishe mwenzio kila uvumi ukoonyesha kumwamini na kumpa nafasi ya kukupa ufafanuzi

8. Kila mahusiano huja na Baraka zake na huondoka na Baraka zake, unaweza ona unapata mafanikio sasa kwa sababu ya kuwa na huyo uliyenaye. Hivyo jitahidi kuzitazama kwa makini kila fursa njema upatazo na ona je zikiondoka utakuaje

9. Fedha huleta ufahari lakini kamwe haina mchango katika kuleta furaha kwenye mahusiano yenu, hivyo pendaneni kama vile ni matajiri na maskini, kwani fedha yaweza kupotea muda wowote na kama mnapendana itarudi pia kwa kushirikishana jinsi ya kuirudisha lakini mapenzi yakiisha hata uwe na gunia la pesa ni kazi bure sawa na kuirudisha ladha ya chumvi siku ikiisha

10. Mahusiano ya wawili hupendeza kama hayataingiliwa na watu wengine nanyi mkishirikishana katika kutatua matatizo na kuwa na maamuzi ya pamoja kwa kila jambo

11. Ni vyema kutengeneza mazoea ya kujivunia na kuona ufahari kwa huyo uliyenaye na kama ukishindwa kuyafanya hayo kwa huyu hata ukimpata mpya mchezo utakuwa huo huo kwani bado huna ujuzi wa kuishi na mwenzanko

12. Huitaji kuwa dikteta kwa kuwa na misimamo ya kikoloni bila ya kuwa na utambuzi wa kuwa mko watu wa wili hivyo acha tabia za ubinafsi



13. Wanawake wazuri na wanaume wenye mvuto hawawezi kwisha amini uliyenaye hukumpata kwa bahati mbaya , mpende kwa dhati

14. Kila maamuzi ufanyayo sasa ukiwa na stress au huna sress huwa na tabia ya kuihaibu kesho yako, hivyo jitahidi kuwa na subira katika kila jambo

15. Mapenzi hayaonyeshwi kwa kuvungua zibu au kwa binti kutyanua miguu tuu, mapenzi ni hisia, jinsi mnavyoishi, maelewano, ushirikiano na mambo mengine mengi

16. Upendo hausubiri siku ya valentine, kila siku ifanye kuwa siku ya valentine kwa mpenzi wako

No comments:

Post a Comment