Mke anapomjali na kumkubali mume humuongezea kujiamini…
Mahusiano
kati ya mume na mke nyumbani huweza kumfanya mume afanikiwe kwenye
shughuli zake au aanguke. Kwa nini? Ni kwamba, mtu ambaye anakataliwa na
mtu au watu wanaomhusu huwa anakosa kujiamini, huwa anafikia mahali
ambapo hujichukia hata yeye mwenyewe.
Mke anapomkosoa mume,
anapomlalamikia kila mara na kuwa na ghubu, bila kujali kama mume huyo
amekosa au hapana, mume hufikia mahali huanza kujitilia mashaka kama
kweli ana uwezo wa kufanya mambo, kama kweli ana thamani anayodhani kuwa
anayo. Kujiuliza huku mara nyingi kuna maana ya mwanaume kuanza
kupoteza kujiamini na hata kuanza kuwa na uhusiano mbaya na watu
anaohusiana nao mahali pengine kama kazini. Unaweza kumgundua mtu ambaye
ana mke mlalamikaji, mkosoaji na mwenye ghubu kwa kuangalia jinsi
anavyojitathmini.
Kama mke ni mkosoaji na mwenye ghubu kwa mumewe ni
lazima mume atakosa kujiamini katika kufanya mambo yake mengi, ni lazima
ataanza kuwa na uhusiano mmbaya na watu wengine kutokana na hukohuko
kutojiamini kwake ambako kumesababishwa na ghubu na kukosoa kwengi kwa
mkewe. Mwanaume ambaye ana mke mkosoaji na mwenye ghubu hutokea
kutowapenda watu wengine na kukosoa wengine inatokea kuwa sehemu muhimu
kwa maisha yake, anatokea kuwa na hasira za karibukaribu na ni vigumu
sana kwa mtu wa aina hii kuelewana na watu.
Baadhi ya makampuni huko
Marekani, kabla hayajampandisha mtumishi wake cheo, humchunguza mke wa
mtumishi. Hawachunguzi kama ni mzuri wa sura au kama anajua mapenzi au
kupika vizuri. Mara zote huchunguza kama mwanamke huwa anampa mumewe
moyo, kama hamkosoi na kumlalamikia na kama hana ghubu. Wanapogundua
kwamba mke wa mtumishi siyo mkosoaji
wala mwenye kulalamika-lalamika
humpa cheo mtumshi kwa imani kwamba atakuwa ni mtu mwenye kujiamini.
Lakini wanapogundua kwamba mke ni mwenye kukosoa, mwenye ghubu na
mlalamikaji, kamwe hawampi mtumishi cheo, kwa sababu wanaamini kwamba, mtumishi huyo hawezi kuwa makini, atakuwa hajiamini.
Swali langu hapa je hii ni pale tu mwanamke anapomjali mume na ndio iwe
hivi? Je? mwanamke astahili kujaliwa na kukubaliwa ili kuongeza
kujiamini?..au ndo kusema mwanamke anajiamini sana kuliko mwanamume?..
No comments:
Post a Comment