Bunge la katiba likiendelea mjini Dodoma.
Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa NLD - Zanzibar, Khamis Haji Mussa katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari mjini hapa juzi, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Dk Emmanuel Makaidi amewasilisha majina mawili, la kwake na la mkewe, Modesta Ponera kwa ajili ya uteuzi.
Chama cha National League for Democracy (NLD) Zanzibar kimemtaka, Rais Jakaya Kikwete kufuta uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia chama hicho kwa madai kuwa walioteuliwa katika chama hicho ni mtu na mkewe na kufanya uteuzi huo kukosa sura ya Muungano.
Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa NLD -
Zanzibar, Khamis Haji Mussa katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya
habari mjini hapa juzi, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Dk Emmanuel
Makaidi amewasilisha majina mawili, la kwake na la mkewe, Modesta Ponera
kwa ajili ya uteuzi.
Alisema NLD - Zanzibar kilianza kufuatilia
taratibu za uwasilishaji wa barua tangu Desemba 27, mwaka jana kwa
kumwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ baada ya kupokea maelekezo
ya Ikulu ya Tanzania kwamba majina ya Zanzibar yatafanyiwa kazi
visiwani na ya Bara yangepelekwa Ikulu Dar es Salaam.
Alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, vyama vyote
vyenye usajili wa kudumu vilitakiwa kila kimoja kutoa mtu mmoja kutoka
Tanzania Bara na mwingine Zanzibar ili kuwa na sura ya kitaifa, lakini
Dk Makaidi alikiuka utaratibu huo.
Makaidi ajitetea
Akizungumzia tuhuma hizo, Dk Makaidi alikiri kuwa
Ponela ni mke wake, lakini akasema ni mwanachama wa NLD, hivyo ana haki
ya kuteuliwa.
Alisema alipeleka majina manne Ikulu na kwamba
upande wa Zanzibar ulitakiwa kufanya hivyo kupitia Ikulu ya Zanzibar...
“Walifanya uzembe, hawakupeleka majina ya wanachama wa NLD, matokeo yake
nikapeleka majina manne, tukapata uwakilishi.”
Alisema mkewe ni mwanachama wa NLD hivyo ana haki
ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yoyote kulingana na sifa
zake... “Wanalalamika nini hata chama tawala cha CCM, Rais Jakaya
Kikwete ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mkewe Salma pia
ni mjumbe wa Nec.”
Alisema Ponela kuwa mkewe hakumfanyi akose haki zake za msingi na kwamba sifa zake na elimu ndivyo vilivyomfanya Rais amteue.
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Florens Turuka
alipoulizwa alisema Ikulu haina taarifa za suala hilo lakini wanaamini
vyama vya siasa vilikaa na kupendekeza majina manne na kuyawasilisha
Ikulu, ndipo Rais alipoteua wajumbe mawili kati yake.
Mzimu wa posho walitesa Bunge la Katiba
Siku mbili baada ya kuanza kwa Bunge hilo, baadhi
ya wajumbe wametaka waongewe posho kwa maelezo kuwa kiasi wanachopewa
sasa cha Sh300,000 kwa siku hakiwatoshi kutokana na kupanda kwa gharama
za maisha Dodoma.
No comments:
Post a Comment