Ni
elimu ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo kwamba kutofautisha maeneo ni
jambo la busara. Kwamba sura yako iwe nyingine unapokutana na watu wa
mitaani, itofautiane unapokuwa na wazazi, vivyo hivyo pale ambapo upo
sehemu ‘spesho’ na mwenzi wako.
Lazima uwe unabadilika kama kinyonga. Ukiwa kazini mbele ya watu
unaowaongoza unazungumza kwa sauti ya amri, lakini hiyo hupaswi kuitumia
unapokuwa na wazazi wako. Unaongea kwa sauti kali ya kuamrisha mbele ya
baba yako, hiyo adabu umefundishwa wapi?
Kuna lugha ya kuzungumza ukiwa na mwenzi wako. Ni mwiko kutoa sauti
ya kuamrisha. Ni vizuri kumnyenyekea lakini si katika kiwango ambacho
kitakufanya uonekane una kasoro za
kisaikolojia. Tawile kwa kila
linalosemwa na mpenzi wako hairuhusiwi, unatakiwa kuweka mbele hisia
zako.
Upole kupitiliza hauna maana kwamba wewe ni mpenzi sahihi. Eti,
utaonekana una nidhamu na unamsikiliza vizuri mwenzio, la hasha!
Utatambulika kuwa mtu hai kulingana na jinsi akili yako inavyofanya
kazi. Namna hisia zako zinavyoonesha uhai unapogushwa na matukio
mbalimbali ndivyo na ubinadamu wako unavyosomeka.
Unahoji mambo kwa sauti yenye ujazo wa kutosha, unachukia pale
unapoona mambo hayajaenda sawa, unaumia pale unapotendwa na unafurahi
mipango inapokuwa chanya. Hii ndiyo mantiki ya kukutaka uwe na akili
hai. Itashangaza umepata habari kwamba mwenzi wako yupo gesti na mpenzi
mwingine halafu utabasamu.
Sumu hatari inayosababisha mmomonyoko wa ndoa au uhusiano wa
kimapenzi kwa watu wengi ni kushindwa kujipanga kimaeneo. Ratiba za
ofisini kuingiza nyumbani. Marafiki kuathiri taratibu za mapenzi yenu,
ingawa kila kitu kina umuhimu wake kulingana na wakati husika.
Umeudhiwa na wafanyakazi wenzako kazini, unatakiwa kuweka hekima
mbele. Unarudi nyumbani ukiwa na imani kwamba huko utakutana na mwenzi
wako na ndiye mfariji wako. Kichwa kizito, basi mueleze mwenzio ajue
kinachokusibu kuliko kumpa majibu ya mkato. Itakuharibia badala ya
kukusaidia.
Ukirudi umenuna, mwenzio anakusemesha umekunja ndita ni kosa kubwa.
Na kama utashindwa kujirekebisha inaweza kukusababishia kasoro za
kimaumbile. Utaonekana mkorofi kumbe ni kosa la kutokujipanga.
Haiwezekani kibano ulichopewa ofisini na bosi wako, hasira uzimalizie
nyumbani.
Hii ndiyo sababu ya kukutaka ujifunze kuweka maudhi ya pembeni kando
unapokuwa na mwenzi wako. Unapovuka kizingiti cha mlango, hakikisha
hasira zote unaziacha hapo ili unapoingia ndani kichwa chako kiwe
chepesi kupokea yaliyomo ndani ya nyumba.
Inahitaji hekima za hali ya juu kusahau maudhi ya nje haraka, kwani wengi wamekuwa shubiri kwa wapenzi wao. Anaingia ndani, mwenzake anampokea kwa bashasha lakini badala ya kumpokea, anamsukuma! Kitu kidogo anafoka: “Usinitibue, kichwa changu hakipo sawa leo.”
Inahitaji hekima za hali ya juu kusahau maudhi ya nje haraka, kwani wengi wamekuwa shubiri kwa wapenzi wao. Anaingia ndani, mwenzake anampokea kwa bashasha lakini badala ya kumpokea, anamsukuma! Kitu kidogo anafoka: “Usinitibue, kichwa changu hakipo sawa leo.”
Nimeeleza kuwa inahitaji mtu mwenye hekima ya kiwango cha juu kuweza
kuepuka hasira za pembeni anapokuwa na mwenzi wake. Ni moyo wa kishujaa
kweli, kwani wengi moto wan je huuwasha ndani mpaka nyumba inashindwa
kukalika.
Inawezekana kiwango cha uvumilivu ni kidogo, kwahiyo ni ngumu
kutenganisha maudhi kwa haraka, hivyo hapa chini kuna njia sita ambazo
zinaweza kukusaidia kukabiliana na hali hiyo pale yanapokufika.
Inahitaji hekima za hali ya juu kusahau maudhi ya nje haraka, kwani
wengi wamekuwa shubiri kwa wapenzi wao. Anaingia ndani, mwenzake
anampokea kwa bashasha lakini badala ya kumpokea, anamsukuma! Kitu
kidogo anafoka: “Usinitibue, kichwa changu hakipo sawa leo.”
Nimeeleza kuwa inahitaji mtu mwenye hekima ya kiwango cha juu kuweza kuepuka hasira za pembeni anapokuwa na mwenzi wake. Ni moyo wa kishujaa kweli, kwani wengi moto wa nje huuwasha ndani mpaka nyumba inashindwa kukalika.
Inawezekana kiwango cha uvumilivu ni kidogo, kwa hiyo ni ngumu
kutenganisha maudhi kwa haraka, hivyo hapa chini kuna njia sita ambazo
zinaweza kukusaidia kukabiliana na hali hiyo pale yanapokufika.
MUELEZE HUJISIKII VIZURI
Ikibidi sema unaumwa. Mpenzi bora atapunguza maswali au baadhi ya vitu na kukuacha upumzike. Hiyo itakusaidia kuingiza hewa kichwani ambayo itakuongezea nafasi na mwisho wa siku kichwa kitakuwa chepesi.
Maneno ya hapa na pale ukiwa na msongo wa vitu kichwani, utaona kama ni vuvuzela zinapuliza masikioni. Unapomuomba mwenzio akupe nafasi ya kupumzika kwa sababu hujisikii vizuri, itakusaidia kupunguza uzito wa kichwa.
ANGALIZO; Unapaswa kuwahi kujieleza kabla mwenzako hajaanza yake, kwa maana akisema yeye halafu wewe ndiye ufuate, atajua umeamua kumkwepa.
LALA USINGIZI
Tafuta usingizi kisha utokomee kwenye njozi, ukiamka hutokuwa yule yule. Angalau kichwa kitakuwa kimepumua na uzito umepungua.
EPUKA MAJADILIANO
Kama nilivyosema mwanzo, unapokuwa na vitu vingi kichwani halafu uendelee kuongeza vingine utaona ni sawa na vuvuzela zinapuliza masikioni. Hivyo basi, itakuwa nafuu kwako endapo utakataa majadiliano ya aina yoyote.
Kuepuka majadiliano, siyo tu kwamba kutaleta unafuu kichwani, bali pia kutakuepusha na migogoro ambayo unaweza kuingia kwa sababu ya msongo.
MUELEZE KINACHOKUSUMBUA
Ni tiba kwako endapo utafungua kinywa na kumueleza mwenzio kile ambacho kinakusumbua. Atajua kinachokusibu, kwa hiyo atajua jinsi ya kukuzoea kuliko kufika na kukaa kimya au kumjibu mkato au kufoka bila mpango.
CHAGUA KINACHOKUFURAHISHA, FANYA
Unapenda kuangalia filamu au kingine chochote na unaamini ukikifanya kitakuondolea hasira, basi fanya ili kujiweka vizuri kisaikolojia mbele ya mwenzi wako. Kuna wale ambao hasira zao hutoweka baada ya kupanda kitandani, nalo si tatizo ilimradi kutibu hasira.
Angalizo ni kwamba kupanda kitandani kunahitaji uhuru wa hisia. Utazungumza vipi na mwenzi wako mpaka mkubaliane kupeana hiyo dawa? Muhimu ni kumueleza kinachokusibu, akikuhurumia, basi huo ndiyo uwe mwanzo wa kutii kiu.
UVUMILIVU
Yote ni muhimu, lakini uvumilivu ni kitu cha msingi. Jifunze kusikiliza vitu bila kutoa majibu. Acha baadhi ya mambo yawe fahari ya masikio. Inawezekana umesikia na jibu unalo lakini unatakiwa uitambue hali uliyonayo, kwa hiyo endelea kunyamaza.
Ukiweza hili basi umefaulu mtihani mgumu na haitatokea ugombane na mwenzio kisa umeudhiwa na kazini kwako au kwenye daladala.
No comments:
Post a Comment