Bunge la Kenya lenye wabunge
wengi wanaume limeidhinisha mageuzi yenye utata katika mswada wa ndoa
ambayo yatawapa wanaume usemi zaidi katika familia na uhusiano mwingine
katika jamii.
Wabunge wanaume walipitisha mswada mpya wa ndoa baada ya kuufanyia mageuzi na kuruhusu wanaume kuoa zaidi ya mwanamke mmoja bila ya kushauriana na mke wa kwanza. .
Wabunge wanawake waliondoka katika kikao hicho kwa hasira wakiahidi kuubadili mswada huo.
Pia sehemu za sheria ya ndoa ambazo zinasema kuwa wanandoa waweze kugawana mali yao wanapoachana imelegezwa.
Mmoja wa wabunge wanawake alisema kuwa ni muhimu mageuzi hayo katika mswada huo kutupiliwa mbali kwa ajili ya kulinda familia.
''Ni muhimu kumuomba mkeo wa kwanza ruhusa kabla ya kuoa mke wa pili,'' alisema mbunge huyo. Lakini mbunge mmoja mwanamume, Benjamin Washiali, alisisitiza kuwa yeye ni mtoto wa mke wa pili katika familia yao. ''Ikiwa sheria hii ingekuwepo mimi nisingezaliwa.''
Wabunge wengi wanaume wamesema kuwa ni jambo la kawaida kwa wanaume wa kiafrika kuwa na wake zaidi ya mmoja.
Wanawake bungeni sasa wanasema watajitahidi kuhakikisha kuwa mswada huo unatupiliwa mbali.
No comments:
Post a Comment