Utafiti
uliofanywa na chuo kikuu cha Gothenberg, Uswizi, wanaume wengi huwapuuza
wachumba wao wanapoburudishana faraghani.
Utafiti
huo unasema wanaume huongozwa na ubinafsi wanaposhiriki tendo la ndoa na
kusahau kwamba wachumba wao wana hisia.
Kulingana
na utafiti huo wa 2009, ingawa wanaume wengi wanaelewa umuhimu wa kuwandaa
wachumba wao kabla ya kuanza burudani,hawajali yanayowapata wenzao wasipopata
shibe la ngoma.
“Suala
la wanaume kutowaridhisha wapenzi wao linatokana na kukosa kuwaandaa vyema.
Mwili wao husisimka haraka wanapopandwa na hamasa ya kushiriki tendo la ndoa.Wanasahau
kwamba mwili wa mwanamke ni tofauti,” yasema sehemu ya utafiti huo.
Watalaamu
wa masuala ya mapenzi wanasema mwanaume mwenye tabia hii huwa hawezi kumfikisha
mwanamke kileleni.Wanasema ni wazi kwamba mwanamke asipoandaliwa vyema, hawezi
kufurahia burudani.
“Tabia
hii ya wanaume imefanya watemwe na wachumba wao. Wanawake wanataka mwanaume
anayetambua na kuelewa hisia zao, sio wa kuwatumia kama chombo cha kutimiza
haja zake za kimwili bila kujali wanavyohisi,” asema mwanasaikolojia Ronald
Jameson.
Anasema
mwanaume anayeanza kufanya mapenzi kwa pupa, hawezi kujizuia kufunga bao baada
ya sekunde chache na kumuacha mpenzi wake akitamani burudani.
“Huwa
vigumu kwa wanaume wa aina hii kurudia ngoma jambo ambalo wanawake wengi
huchukia” asema.
Wataalamu
wengi wa mapenzi wanabainisha kwamba wanaume wanaotumia muda mwingi kuwaandaa
wachumba wao kwa burudani, huweza kujizuia kufunga bao mapema na hivyo
hufanikiwa kumfikisha mwanamke kileleni zaidi ya mara moja.
Kujali
hisia
“Uhusiano
wa aina hii ambapo wanaume wanajali hisia za wapenzi wao hudumu kwa muda mrefu,
furaha utawala na mapenzi hunoga huku kila mmoja akimwaza mwenzake kila wakati
na kutamani burudani zaidi,” aeleza Jameson.
Anasema
mbinu na muda wa kumwandaa mwanamke hutegemea mtu binafsi.
“Kuna
wanawake wanaosisimka wanapoguswa sehemu tofauti za mwili na wengine hupandwa
na hamu ya kufanya mapenzi wanapobusiwa. Wengine wanaingiwa na hamasa kwa
kumtizama mwanaume anayewavutia” asema.
Wataalamu
wanawakosoa baadhi ya wanawake kwa kuchangia misukosuko ya mapenzi hasa kukosa
shibe la burudani kwa kutowaongoza wanaume wao kwa maneno ama kwa kuweka mikono
eneo wanalotaka washikwe ili kuamsha hisia zao za mapenzi.
“Ni
rahisi kwa mwanamke kufanya mchumba wake ashindwe kusakata ngoma ipasavyo kwa
kutoshiriki kikamilifu katika mechi kitandani” asema.
Wataalamu
wanasema baadhi ya wanawake huwa hawana ujasiri wa kumwongoza mwanaume
kumtomasa sehemu inayoamsha hisia zake za kufanya mapenzi. Jambo hili, asema
Jameson, huwanyima raha ya burudani na kusambaratisha penzi. Hata hivyo ili
kumwandaa mwanamke wa aina hii, watalaamu wanasema mwanaume anapaswa kutumia
ujuzi wa hali ya juu ili kuamsha ashiki zake.
Ili
zoezi la kusakata ngoma lifanikiwe na kufanya uhusiano wa mapenzi huwe thabiti,
mwanamke anatakiwa kuonyesha ushirikiano kwa kutoa miguno na minongono ya
kumchanganya mwanaume.
Kulingana
na utafiti wa chuo kikuu cha Gothenberg, wanawake hawaridhishwi na tabia ya
wapenzi wao kupuuza umuhimu wa kuwaandaa kabla ya kufanya mapenzi.
Watafiti
wanasema wanawake wanachukia wanaume wenye pupa ya kufanya mapenzi. Na huenda
afueni isipatikane kuhusu hali hii huku wanaume wakiwalaumu wanawake kwa kukosa
uwazi katika swala la mapenzi kwa kutowaeleza wanaume kwamba hawako tayari.
Kukubaliana
na utafiti
Wanawake
wengi nchini walikubaliana na utafiti huo wakisema unaeleza jinsi mambo
yalivyo. Wanafananisha hisia za mapenzi za mwanaume na jiko linalotumia mafuta
ya taa linalowaka kwa haraka kisha kuzimika, na mwanamke na jiko la makaa
linalochukua muda kuwaka na halizimiki kwa haraka.
“Mwanamke
ni sawa na jiko la makaa linalohitaji bidii kulichochea liwake, na likishawaka
ni kazi ngumu kweli kulizima,” asema Bi Ruth Wanjiku.
Mwanadada
huyu anakiri ushirikiano wa hali ya juu ni muhimu kufanikisha burudani
kitandani .
“Ni
kweli wanaume wana haraka ya kufanya mapenzi na humaliza shughuli hata kabla ya
mwanamke kuanza kuwaka. Hata hivyo baadhi ya wanawake wanachangia kwa
kutoshiriki kikamilifu wanaporushana roho,” asema Bi Wanjiku.
Anakubaliana
na watafiti waliofichua kwamba wanawake wanachangia kufanya wanaume wapungukiwe
na nguvu za kufanya mapenzi kwa kutohusika ipasavyo.
“Ni
muhimu kwa wana ndoa au wapenzi kufahamiana vyema ili waweze kusisimuana,”
aeleza Bi Mary Kituyi mkazi wa jiji la Nairobi. Anasema wapo wanaume wasiowapa
wachumba wao nafasi ya kuonyesha ustadi wao wa kurushana roho
“Kuna
wanaume wanaoamini kwamba mwanamke hafai kumfundisha mambo ya mapenzi.
Ukijaribu kumwelekeza unakotaka uguswe au mbinu unayofurahia anaanza ugomvi,”
anasema na kuongeza kwamba uhusiano wa aina hii hauwezi kudumu.
Kulingana
na mwanasaikolojia Peter Obonyo wachumba wanaokabiliwa na tatizo hili wanaweza
kulisuluhisha bila ya kuachana.
“
Dawa la tatizo hili sio kumwacha mchumba wako, mbali ni kumzungumzia kwa lugha
ya mapenzi na sio kwa ukali,” asema.
Anashauri
wanaokabiliwa na tatizo hili wasome vitabu au majarida yanayotoa elimu juu ya
kufanya mapenzi na wataalamu wa mapenzi kwa ushauri.
“
Wakishapata elimu ya kutosha na kuizingatia, watajitayarisha kisaikolojia na
utashangaa mwanamke anafika kileleni kabla ya mwanaume. Hakuna miujiza hapa, ni
mambo ya kisaikolojia tu,” asema.
Kulingana
na mwanasaikolojia huyu wanaowaacha wachumba wao kusaka shibe la mapenzi,
hukabiliwa na hatari nyingi.
“Wanaweza
kugeuka kuwa wahamaji wa mapenzi kwa kubadilisha wachumba kila mara. Pia kuna
hatari ya kuathirika kisaikolojia na kukosa utulivu wa kihisia,” asema.
Maandalizi
ya mapema
Kulingana
na wataalamu mawasiliano ni muhimu kati ya wapenzi ili kila mmoja aweze kumwandaa
mwenzake vyema na kwa upendo kabla ya kushiriki tendo la ndoa.
“Maandalizi
huwa kwa njia nyingi.Mazungumzo yenu, usafi wa nguo, mwili na chumba murua cha
kuandalia burudani ni muhimu,” asema na kuongeza kwamba mwanaume anafaa
kuonyesha utulivu na kujali hisia za mpenzi wake.”
Pia
mwanamke hafai kuona aibu kumuongoza kipenzi chake ili wafurahi pamoja.
Kulingana
na Bi Wanjiru mwanamme mwenye upendo hufurahi sana ikiwa mpenzi wake atafunua
hisia zake. Anasema kwa kawaida si rahisi wanawake kuelezea hisia zao kwa
maneno na wanaume wanafaa kufahamu ishara za wachumba wao wakiwa tayari
kuteremka katika bahari ya mapenzi.
No comments:
Post a Comment