Watu wengi tuna desturi ya kula ili tushibe. Katika ulaji
huo wakati mwingine tunajitendea ukatili wenyewe kwa kula vyakula
visivyo sahihi ambavyo vinapoingia mwilini hugeuka kuwa sumu.
Lakini vyakula pia ni dawa na leo tutajua, japo machache,
juu ya namna gani vyakula ni dawa yenye uwezo wa kutibu maradhi, hata
yaliyoshindikana hospitalini.
Vyakula ni tiba duniani toka enzi. Miongoni mwa mabingwa wa tiba za vyakula ni watu wa jamii ya Wachina toka Tibet waitwao ‘Tibetans’ au ‘Watibeti’. Hawa walianza kutoa tiba kwa kutumia vyakula miaka mingi sana na hadi leo ukifika Tibet utakutana na tiba hii maarufu kama ‘ Tibetan Food Theraphy’ ambayo imeanza kuenea nchini hivi sasa.
Tiba ya vyakula haihitaji utitiri wa madaktari na wauguzi
kwa kuwa mgonjwa na daktari huonana mara moja kwa mwaka au miwili kwa
kuwa daktari humsikiliza mgonjwa, humpa maelekezo juu ya kula aina
fulani za vyakula ili apone na mgonjwa hufuata maelekezo hayo rahisi na
yanayoeleweka kisha mgonjwa hupona.
Katika maelekezo ambayo madaktari wa lishe huwapa wagonjwa
kubwa nikwamba mgonjwa anatakiwa aache tabia ya ulafi. Mgonjwa anatakiwa
ale wastani wa robo tatu ya ujazo wa tumbo lake kwa uwiano, chakula
kiwe nusu na kinywaji kiwe robo, ili tumbo lipate nafuu ya kuyeyusha na
kufyonza virutubisho kirahisi toka katika chakula.
Pia maelekezo huwa mengi kwa baadhi ya wagonjwa mfano wengi
wetu tunakula mlo mmoja tu na kudhani kulikopa tumbo ni kawaida kumbe
ni kusababisha maradhi, kwani hutalitendea haki tumbo kwa kula mara moja
kwa siku.
Kwa mfano, ukila matunda na mboga mbichi zisizopikwa
(saladi/ kachumbari) basi uyeyushaji na ufyonzaji wa virutubisho huwa
rahisi, tumbo huchukua saa 13 tu kukamilisha kazi hiyo. Ila, ukivipika
vyakula hivyo basi ujue tumbo litagharimu saa 24 kukamilisha kazi ya
ufyonzaji wa chakula hicho.
Tumbo hukutana na kibarua kigumu pale tunapokula vyakula vyenye asili ya usindikaji, nyama, vyakula vilivyopikwa kwa mafuta nk. Kwani hujikuta likihangaika na kazi ya usagaji kwa takriban saa 72 ambayo ni karibu siku tatu.
Hapo ndipo tumbo huweka kando sumu za vyakula hivyo. Sumu
zitokanazo na mafuta mabaya, lehemu, chumvi, caffeine na tindikali
mbalimbali huanza kulishambulia ini ambalo ndilo ‘Benki kuu’ ya mwili wa
binadamu na hapo ndipo mifumo mingine huathirika na mtu kujikuta
akiugua maradhi ya moyo na damu kama vile shinikizo la damu, kisukari na
kupooza.
Aina nyingi za saratani huanzia hapo hivyo mtu kujikuta
akitafuta msaada wa tiba ambayo kwa kiasi kikubwa madawa pamoja na
mchanganyiko wa vitamin mbalimbali huhusishwa katika matibabu. Lakini
pia maumivu toka tumboni, tumbo kujaa gesi, kukosa haja kubwa kwa muda
mrefu na hata kukosa hamu ya kula.
Tumbo huweza kuhifadhi vyakula vyote unavyokula kila siku
huku vingine vikikaa tumboni kwa saa 72 bila kuyeyuka kwa sababu utumbo
mwembamba tu wa binadamu una urefu wa futi 22 au mita saba, sawa na
urefu wa nguzo ya umeme. Utumbo huo umeungana na utumbo mnene. Huu una
urefu wa futi 5 au mita moja na nusu.
No comments:
Post a Comment