Hii ni story ambayo kila nikiisoma waga machozi yananitoka. ivi
unafikili asingekuwa mama yako ungelikuwepo duniani humu? ebu fuatilia
story hii kisha mwisho unambie nani kama mama yako.
alijitahidi kula vyakula bora, kulala kwenye chandarua chenye dawa ili
usipatwe na ugonjwa wa maralia pindi ulipokuwa bado uko tumboni mwake,
alijitaidi kula vyakula vyenye virutubisho vya kutosha ili uzaliwe na
afya njema, alikula mboga za majani, matunda na kujiepusha na ufanyaji
wa kazi nzito ili wewe uzaliwe ukiwa salama salimini. story haishii hapo
bado inaendelea kama ifuatavyo.....
wewe ulikaa tumboni mwa mama yako miezi tisa, na ilipofika siku ya
mwisho mama yako hakubana miguu yake ili ukauwawe, alichokifanya
alijitahidi kadri awezavyo mpaka ukazaliwa. kipindi chote hicho mama
yako alikumbana na mambo mengi sana ikiwemo (a) kuugua mara kwa mara,
(b) aliumwa sana kwa uchungu mpaka mda mwingine alimpiga makofi baba
yako, nk. lakini yote haya ni kwa ajili yako.
Haikutosha, alikulea kwa shida na taabu, alikuwa tayari kwa lolote
litakalo tokea juu yako, japo familia inajengwa na watu wawili kwanza
ambaye ni baba na mama, lakini mama ameumbwa akiwa ana majukumu mengi
sana zaidi ya baba. Ebu jiulize mpaka kufikia hapo ulipofika ivi nihaki
kabisa
1. Kunyanyua mkono wako na kuanza kupigana na mama yako?
2. Unashindwa hata kumpa kazawadi mama yako japo ata katakuwa hakana thamani kubwa?
3. Unashindwa hata kumjulia khali mama yako?
4. Leo hii eti unanyanyua mdomo wako kisha unaanza kutukanana na mama alio kuzaa ivi kweli?
Japo hauna kipato kikubwa, lakini jitahidi kugawana kile kidogo
ulichonacho wewe na amama yako pamoja na familia yenu kwa ujumla, lakini
mama mpe kipaumbele zaidi ya watu wengine duniani, usimwachie kila kitu
kiwe juu yake yeye mwenyewe, iyo haitokuwa tabia nzuri kabisa
nakwambia.
Hakuna kama mama na haitokuja kutokea hapa duniani, jitaidi kumpenda
zaidi mama yako mzazi. Nakama hauna maelewano mazuri na yeye, ebu jaribu
chukua hatua ya kujiuliza nini chanzo cha kufarakana baina yako na mama
yako, kisha mfuate kwa upole na umuombe msamaha, ili ujiondolee lahana
ya wazazi, ninaimani ya kwamba hata kama ulimkosea makosa 100 atachukua
sekunde 10 tu ambazo ndizo atakazo zitumia kukwambia kuwa mwanangu,
nimekusamehe kabisa tena kwa roho moja.
No comments:
Post a Comment