Friday 18 July 2014

HIZI NDIZO SABABU ZA NDOA ZA WATU WALIOPENDANA SANA NA KUTUMIA GHARAMA KUBWA KUACHIKA!....



 Kwenye suala la kuachika/acha/achwa haliegemei sana kwenye kuyajua mambo kitandani, kwani Ndoa au Mahusiano sio Ngono pekee Natambua kuwa Makungwi wengi wa "Kizazi Kipya" wanafunza mwanamke kuonyesha mapenzi na mavituzi ili asiachwe....na sio Maisha ya Ndoa, Uzazi n.k.  

Nadhani "ukitaka usiachwe" ni "Brand" inayouza sana....kwasababu kila mtu hataki kuachwa au hataki Ndoa yake "ifeli" ndani ya miaka michache....wote wanataka Ndoa zao zidumu muda mrefu. Lakini wanasahau kuwa umri mkubwa wa Ndoa au Uhusiano sio kielelezo cha furaha au mafanikio kwenye Ndoa husika. Baadhi huendelea kubaki kwenye Ndoa kwa sababu nyingine na sio Mapenzi, wengine huendelea kubaki kwenye ndoa kwa vile wanadhani umri mfupi wa Ndoa zao ni aibu kwenye jamii n.k.  
 Ili Uhusiano au Ndoa iwe yenye furaha inahitaji Nguzo kuu 5 ambazo ni Maelewano/Makubaliano, Mawasiliano, Heshima, Uvumilivu na Ushirikiano....Mengine yote hujitokeza humo. 
 Nguzo moja kati ya hizo ikikosekana hakika Ndoa au Uhusiano utayumba. Sasa mmoja asipotoa Ushirikiano kwenye Mawasiliano ili kuwe na Maelewano, amani na furaha hutoweka.  
 
 Hata kama unayajua sana Mambo kitandani, huwezi kuendelea kuishi na mtu asiekupa ushirikiano, asie kuheshimu, kukupenda n.k. Kama umejitahidi kufanya yote au mengi uliyofundwa kama mke lakini Mume haonyeshi kuelewa au kutaka kubadilika ili muendelee kufurahia Muungano wenu then ni bora kutoka Ndoani. Hivyo nadhani hao Makungwi ndoa zao zimefeli kwa sababu nyingi tofauti lakini wapo ni kutokupata ushirikiano kutoka upande wa pili. 
Kwasababu mwanamke kafundwa haina maana ndio awe mtekerezaji wa mahitaji yote muhimu kwenye Ndoa. 

Ndoa ni umoja, Ndoa ni Timu....ndoa ni kuwa tayari kujifunza na kubadilika inapobidi ili muendane
 
 

No comments:

Post a Comment