Wednesday 23 July 2014

SAIKOLOJIA YA MWANAUME KATIKA MAHUSIANO NA JINSI MWANAMKE ANAVYOWEZA KUITUMIA KULETA AMANI NYUMBANI


 Kuna msemo unasema kuwa "mapenzi yanaongoza dunia" kila mtu anayo haki ya kupenda kwa mujibu wa taratibu mbali mbali za dunia hii. 


Mapenzi ni mazuri kama utazingatia mambo muhimu yaliyo halali mbele za Mwenyezi Mungu. Fahamu njia mbadala za wewe msichana zitakazokusaidia kumfahamu mwanaume ambaye ni chaguo lako; 

1. Wanaume wenye heshima ni walinzi na pia watauhifadhi moyo wako, kulinda hisia zako, kulinda heshima yako na watakupatia msaada wa kiroho, kiakili na ustawi wa kimwili. 

2. Wanaume wasiokuwa na heshima, huchukulia tendo la ndoa kama mchezo tu na kiburudisho, na hivyo wanawake kuwa kama tunzo.  Kamwe usiruhusu hali hii ikutokee. 

3. Usihukumu vitendo au tabia ya mwanaume mmoja aliyekutenda kuwa hiyo ni tabia ya wanaume WOTE, labda kama unataka wanaume WOTE wawahukumu wanawake WOTE kwa tabia mbaya ya mwanamke mmoja. 


4. Wanaume wengi hupenda mama zao, hivyo usiongee kitu chochote kibaya kitakachomuhusu mama yake. 
 5. Kama kweli mwanaume anampenda msichana basi atafanya juu chini ili mambo yote yawe rahisi kwa msichana, kwasababu anaupendo wa dhati kwake. 

 6. Jihadharini!!! Mwanaume anaweza kueneza uvumi kama moto na msichana bila kuchelewa anaweza kuusambaza haraka zaidi. 
7. If a guy likes a girl ,he will always tend to tease her or find a way to talk to her. 
 8. Ili kumuelewa mwanaume, unahitaji kumsikiliza kwanza 

 9. Wanaume hupenda wasichana wenye uzuri na akili kuliko wasichana wenye uzuri na vinguo vifupi tu. 

 10. Kama hutumia muda mwingi kumuelezea mwanaume siri zako, basi punguza kwasababu wanaume huwa hawatunzi kumbu kumbu nzuri kama wasichana. 
Muhimu: Njia hizi zinatumika kwa wale wasio katika ndoa, yani kwa wale walioko katika mchakato wa uchumba. Endelea kutembelea site yetu, utajitambua zaidi

No comments:

Post a Comment