Wednesday 23 July 2014

MBINU NA UJANJA WA KUMPA UMPENDAYE SABABU ZA KUKUFANYA WAKE WA MAISHA!

MACHOZI siyo suluhisho la matatizo. Baadhi ya watu wamekuwa wakilia sana baada ya kukutana na mambo ambayo hawaoni njia za kutokea. Kifupi kulia siyo tiba, zaidi unaweza kuwa unajiumiza badala ya kutafuta utatuzi

 Hata katika suala la ndoa, ambalo linawaumiza vichwa vijana wengi wakati mwingine huwatoa machozi. Ninachotaka kukuambia ni kwamba kulia siyo mwisho wa tatizo, kikubwa ni kutafuta njia za kukomesha machozi yako.
Kufanya hivyo utakuwa umefika mwisho wa machozi na kulalamika kwamba huna mvuto, hupendwi au huna bahati ya kupata wako wa maisha.
Wiki iliyopita nilieleza baadhi ya mambo muhimu kwa wanawake kuyazingatia kama kweli wanahitaji kuingia katika ndoa.
Leo naendelea na vipengele vingine ambavyo kwa hakika vinaweza kuwa tiba ya kweli kwako. Hebu vifuatilie kwa makini, ni imani yangu kwamba, utaingiza kitu kipya ubongoni mwako.
KUWA NA STAHA

Wanaume wanapenda kuheshimiwa, naomba nieleweke wazi hapa, nazungumzia juu ya heshima na siyo kuogopwa! Kumuogopa mtu na kumuheshimu ni vitu viwili tofauti, hivyo ni vyema ukawa na heshima kwa mpenzi wako.
Ninaposema staha, ninakuwa na maana pana zaidi. Hapa nazungumzia juu ya kutambua thamani yake, kumpa nafasi ya kwanza katika mapenzi na kumnyenyekea kama mumeo mtarajiwa.
Ni nani anapenda kuwa na mwanamke wa mabishano, majibizano? Mkorofi? Hakuna. Kwahiyo utakapokuwa na staha, msikivu na unayekubali kuelekezwa, tiketi yako ya kuolewa unakuwa nayo mkononi kabisa.

Anza na hatua hii dada yangu na kwa hakika utakuwa katika ile cheni ya kuelekea katika ndoa, ambayo bila shaka ndiyo inayokuumiza kichwa.
JITOE...
Zipo sifa ambazo ni za lazima mwanamke kuwa nazo ili kumshawishi mchumba wako atamani kufunga ndoa na wewe, lakini ukiwa na sifa za ziada inakuwa bora zaidi kwako wewe, maana unakuwa na asilimia kubwa zaidi ya zile zilizotegemewa.
Sifa ya kujitoa ni kubwa sana, jijengee tabia ya kujitoa kwa mpenzi wako.
Mathalani ana matatizo ya kifamilia, kikazi au binafsi. Kuwa wa kwanza kuyajua na kutaka kumsaidia.
Haina maana msaada wako lazima uwe pesa pekee bali hata ushauri wako tu, unaweza kuwa dawa ya kinachomsumbua na hapo ukazidi kuwa na sifa ya kuwa naye kama mkewe. Hilo linawezekana kabisa, lipo mikononi mwako.

No comments:

Post a Comment