Sunday, 28 April 2013

JE UNA TATIZO LA KUWA NA RANGI MAKWAPANI MAGOTINI NYEUSI????



JE UNAJUA KWAMBA DEODORANT UNAYOTUMIA INASABABISHAJE UNJANO WA KWAPA NA NI DEODORANT GANI NZURI KWA MAKWAPA YAKO? PATA HABARI JUU YA KUZUIA MATATIZO HAYA...


Katika peruzi peruzi zangu leo, nikitafuta njia mbalimbali za kuweza kusafisha madoa katika nguo kabla ya kufua, nilifanikiwa pia kukuta na kusoma njia mbalimbali za kienyeji zinazoweza kusaidia kuondoa rangi nyeusi kwenye makwapa, magoti na kwenye mikono sehemu za nyuma (elbow).

Najua hili tatizo linawakwaza wasichana/wanawake wengi juu ya kuwa na makwapa meusi. Inasemekana kwamba, mara nyingi makwapa huwa meusi 
kutokana na kemikali zinazokuwa kwenye deodorants zinazosaidia kuondoa harufu mbaya ya mwili/jasho la kwapa. Lakini hizo hizo kemikali saa nyingine ndo zinazosababisha makwapa kuwa na rangi nyeusi. Pia hizo kemikali kali zinapochanganyikana na jasho husababisha kupatwa kwa rangi ya njano katika nguo haswa sehemu za makwapa.

Vitu vya kuangalia ukiwa unanunua deodorant na wakati wa kujipaka deodorant:
matangazo ya nyuma ya kopo/box la deodorant
1. Kama unatatizo hili, basi ushauri ni kwamba unatakiwa kununua deodorant zisizo na "Aluminum Compounds." Kumbuka kusoma ingridients kwenye kopo, ili ujue kama hii compound ni moja ya kemikali zilizotumika wakati wa kutengeneza deodorant ama la. Kama ipo kwenye product hiyo basi tafuta product nyingine ambayo haina hii compound. 
2. Ukishaoga, hakikisha umejifuta maji vizuri kwenye kwapa na kwapa ni kavu kabisa hivyo ndo ujipake deodorant.
3. Hakikisha deodorant imekauka kwanza kwenye kwapa kabla hujavaa nguo yako.
4. Unapo shevu makwapa zingatia kutoshevu mara kwa mara na pia shevu taratibu bila kuisugua ngozi ya kwapa (irritate). 

Pia, ili kuondoa weusi wa kwapani, tumia limao ama ndimu nusu na sugulia kwenye kwapa kila asubuhi na jioni. Walio kuwa wakirecomend na kuongelea hii remedy hawakusema ni kwa muda gani unatakiwa kupata hayo malimao ila, kwa jinsi ninavyoona, hii ni kazi ya muda mrefu kama makwapa teyari ni meusi. Natumaini hizi home remediz really do work!!  binafsi sina hili tatizo otherwise, ningekuwa wa kwanza kujaribu kwamaana napendaga kujaribugi vitu haswa home remediz ili kujua kama kweli vinafanya kazi kama watu wanavyosema. 

 
                 Malimao

Haya basi, katika usafishaji wa nguo zenye rangi ya njano makwapani. Wanasema changanya kijiko kimoja cha hydrogen peroxide (liquid), kijiko kimoja cha baking soda na maji kidogo. Chukua mchanganyiko wako na apply kwenye sehemu za njano (jasho) za shati KUMBUKA usiloweke shati ama nguo nzima kwenye huu mchanganyiko bali sehemu za njano tuu zilizosababishwa na jasho. Wacha mchanganyiko huu ukae for about dakika 30 then osha nguo.
Kama umezoea kukausha nguo na mashine inabidi kuanza kuanika kwenye kamba kwamaana moto wa mashine unakomaza madoa kama haya. 


Njia tatu za kuweza kuondoa weusi kwenye Magoti na sehemu za nyuma za mikono (elbows). 
changanya sukari na olive oil katika kibakuli ili kutengeneza bodyscrub yako (kienyeji) - sukari inasaidia kuondoa dead skin cells wakati wa kuscrub/kusugua
Unapo apply hii scrub hakikisha unasugua ngozi (ya magotini, elbow) in a circle motions kama dakika mbili ama tatu
Ukishamaliza kuscrub/kusugua ngozi apply moisturizer yenye deep conditioning kwenye ngozi. Mfano; vasiline yenye cocoa butter deep conditioning (moisturizer ina vitamin E)

Subiri baada ya dakika moja ama mbili hivi baada ya kuapply hiyo moisturizer. Halafu apply mustard oil (provides vitamin A,B & E) . Hii mustard oil, Inasaidia kuondoa weusi na kurudisha rangi nzuri na yakawaida ya ngozi na kufanya ngozi iwe laini. Hakikisha unamassage mustard oil vizuri kwenye ngozi iache kwa dakika 5 ama 10. Halafu osha vizuri na maji ya uvugu vugu ama kitaulo cha uvugu vugu. Unaweza kufanya hivi kila siku jioni ama mara moja kwa wiki.  ngozi na olive oil ni kusaidia kumoisturize the skin.

 Chukua lemon juice (kamua malimao) hii ni natural bleacher kwa ngozi. Apply maji yako ya limao kwenye ngozi na massage/ama sugua taratibu ngozi halafu acha maji hayo ya limao yakae kwenye ngozi kwa muda. Chukua natural coconut oil (kijiko cha chai kimoja) na maji ya ndimu kijiko cha chai kimoja changanya kwa pamoja. Hii pia ni natural bleacher ya ngozi halafu apply kama cream kwenye area ya ngozi uliyokuwa ukiscrub. Acha ikae kwa muda wa dakika 5 hadi 10 halafu osha ngozi. Apply, vaseline cocoa butter deep conditioning (moisturizer) mahali hapo. Nadhani huu mchanganyiko pia unaweza kuapply sehemu za katikati za mapaja kwamaana pia wakati mwingine kutokana na mapaja kusuguana sehemu hizi hubadilika rangi na kuwa nyeusi.






No comments:

Post a Comment