Sunday 28 April 2013

UNAWEZA KUPUNGUZA UNENE KWA VYAKULA HIVI.........

 

NI ndoto ya wasichana wengi wanene kupunguza unene, lakini wengi wao hawajui wafanye nini. Zipo njia nyingi za kumfanya mtu apunguze unene, miongoni mwa njia hizo ni pamoja na vyakula, kujua aina ya vyakula unavyotakiwa kula na kuvila kama inavyoelekezwa.


Tikitimaji.

Vifuatavyo ni vyakula, mboga na matunda ambayo yakiliwa kwa mpangilio mzuri huondoa mafuta ya ziada mwilini na hivyo kupunguza unene wa ziada. Vyakula hivi vina sifa ya kuchoma yenyewe mafuta kabla ya kuhifadhiwa mwilini:

  
                               Machungwa.

MATUNDA
Matunda ni miongoni mwa vyakula vinavyoyeyusha mafuta mwilini, idadi kubwa ya mtunda huwa na kiwango kidogo cha kalori (calories) lakini yana kiasi kingi cha kamba lishe (fibre).
Matunda yenye kamba lishe nyingi huyeyusha mafuta mwilini haraka kwa kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na humuongezea mtu nishati ya mwili. Kwa sababu hii, unaweza kuchanganya ulaji wa matunda na vyakula vyenye mafuta bila kuongezeka unene. Matunda kama epo, machungwa, zabibu, mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiasi kingi cha kamba lishe.


  
                         Mapera.
Vilevile, tikitimaji lina faida kubwa mwilini, kwani lina uwezo wa kuondoa sumu mwilini (toxins) ambayo huingia mwilini kwa njia ya chakula na hewa tunayoivuta kutokana na hali halisi ya maisha ilivyo. Pia tikitimaji linapoliwa huondoa maji ya ziada mwilini, pendelea kula tikitimaji kila wakati unaposikia tumbo kujaa au kuchafuka.





                                                  kabeji

MBOGA ZA MAJANI
Mboga nyingi za majani huwa na kiasi fulani cha kamba lishe, na kamba lishe iko katika makundi mawili, ya kwanza ikiwa ni ile inayoyeyuka mapema na ile isiyoyeyuka mapema, mbogamboga zinazochukua muda kuyeyuka tumboni lakini zinasaidia sana usagaji wa chakula haraka ni pamoja na mchicha, spinachi, kabeji, maharage ya kijani na nyingine jamii ya majani kibichi.
PROTINI
Idadi kubwa ya vyakula vinavyoyeyusha mafuta haraka mwilini katika jamii ya vyakula vya protini ni vyakula vya baharini. Ingawa samaki huhitaji nishati nyingi kuyeyushwa mwilini, lakini ni miongoni mwa vyakula vinavyosaidia uyeyushaji wa mafuta mwilini kwa haraka zaidi. Ili kupata matokeo mazuri na ya haraka, pendelea kula vyakula vya baharini sambamba na mboga za majani kama vile kabichi au saladi ya mbogamboga mchanganyiko.
Vilevile kuna aina nyingine ya vyakula ambavyo vina uwezo mkubwa wa kuyeyusha mafuta ya ziada mwilini kama vile vyakula vitokanavyo na maziwa, ngano isiyokobolewa, wali, ambavyo wakati wa kutayarisha unatakiwa kuhakikisha vinakuwa na kiwango kidogo cha mafuta asilia bila kuongezewa ya ziada. Ukizingatia ulaji wa vyakula vilivyoanishwa hapo juu kwa wingi, bila shaka utapungua mwili au hutaongezeka mwili zaidi ya ulivyo sasa.


No comments:

Post a Comment