Monday 22 April 2013

LEMA MBUNGE HALALI, ASHINDA RUFAA DHIDI YAKE.

 
Mbunge wa Jimbo la Ausha Mjini Godbless Lema akizungumza na wafuasi wake nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mwaka jana.


WAKATI Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akisubiriwa Bungeni kutoa udhibitisho juu ya kauli aliyoitoa bungeni hapo kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni mdini leo mbunge huyo ameibuka kidedea baada ya mahakama ya rufaa kutupilia mbali rufaa iliyokatwa dhidi yake.
Mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi ya marejeo ya rufaa iliyomrejesha bungeni Lema. Maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo na makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha,kupitia kwa mawakili wao Alute Mughway na Modest Akida wakiiomba mahakama hiyo ifanye marejeo ya hukumu yake hiyo, wakidai kuwa hukumu hiyo haikuwa sahihi.
Hata hivyo Mahakama ya Rufani ilisikiliza maombi hayo kutoka kwa waombaji pamoja na hoja za wajibu maombi na kisha kutoa uamuzi uliotupilia mbali maomb hayo, huku ikisema kuwa hayana msingi.
Uamuzi huo wa kutupilia mbali maombi hayo ulisomwa na Jaji Bernard Luanda, kwa niaba ya jopo la majaji wenzake waliokuwa wakiongozwa na Jaji Engela Kileo, pamoja na Jaji Salum Massati.
Hata hivyo jopo hilo halikutoa sababu za kutupilia mbali maombi hayo na badala yeke ikasema kuwa itatoa maelezo ya kina baadaye. Jopo la Majaji hao ukitoa Jaji Kileo pekee ndiyo hakuwepo wakati kesi hiyo na waliobaki wote ndiyo waliosikiliza hukumu ya rufaa iliyomrejesha Lema bungeni, ambayo ilikuwa inapingwa na makada hao wa CCM.

No comments:

Post a Comment