Sunday 28 April 2013

CHADEMA WATISHIA KUMSHTAKI RC-ARUSHA


Mnakumbuka kuwa waliomchukia Yesu walimfungulia mashtaka ya uongo wakamfikisha mbele ya pilato. Walipoambiwa watoe ushahidi wakashindwa, lakini wakapiga kelele asulubiwe. Yesu alipigwa, akatemewa mate, lakini yeye akasema ‘ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke lakini si kama nitakavyo mimi bali mapenzi ya Mungu yatimizwe’.

“Vivyo hivyo Edward, aliposakamwa sana aliamua kujiuzulu uwaziri mkuu...lakini tunajua kuwa Yesu, baada ya kuuawa, alifufuka na kuinuliwa. Naomba kanisa liendelee kumuombea Lowassa ili naye ainuliwe juu katika nchi yetu ya Tanzania,” alisema Lugola
.
Filikunjombe naye alimwaga sifa kwa Lowassa akimtaka kutokatishwa tamaa na maneno yanayosemwa, na kuongeza kuwa siku zote mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe.

Wiki iliyopita katika kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM, Lugola na Filikunjombe walisutwa kutokana na mwenendo wa kuikosoa serikali na kuwashambulia mawaziri.

Mbunge aliyewawashia moto wabunge hao ni Said Nkumba wa Sikonge ambaye alihoji mwenendo wao.
Mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mkumba alisema kuwa wabunge hao wanatumika na CHADEMA na kuwataka waamue kama wanabaki CCM au la.

Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wengi, huku mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akitolea mfano wake.
Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima naye alimbana Lugola ataje majina ya mawaziri alioliambia Bunge kwamba wanauza unga.

Alisema Mulongo amekuwa kikwazo kwao kwa kuwa si mara ya kwanza kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Chadema na kwamba mara nyingine amekuwa akimtuhumu Lema kwa uongo.

Kutokana na mazingira hayo, alisema kama chama hawawezi kupuuzia hali hiyo, sababu itazidi kuwaumiza na huenda wakapachikwa kesi zisizowahusu.

“Hadi sasa tumeshawasiliana na wenzetu ambao ni wanasheria wa Chadema na tutamfikisha mahakamani huyu RC (Mulongo) maana kauli zake ni za kutupinga na sisi zinatuchosha,” alisema

Akizungumzia suala la kukamatwa kwa Lema usiku wa kuamkia juzi, alisema mpaka sasa mlalamikaji katika kesi hiyo hakuna, lakini wanahofia vitisho vinavyodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa kuwa mbunge wao huyo `hatachomoka’ katika sakata la sasa, hivyo kupitia kwa mwanasheria wao wanajipanga kukabiliana na Mulongo.

Awali Wakili wa Lema, Humprey Mtui alisema anashangazwa na kitendo cha polisi kumvunjia heshima mbunge huyo kwa kumkamata mithili ya mtu wa mtaani.

Alisema kwa mujibu wa sheria, Lema alipaswa kuitwa na Polisi lakini kama angekataa, basi ndipo angeweza kuchukuliwa sheria kama hiyo lakini sio kwa kitendo cha polisi, walichokifanya cha kwenda nyumbani kwake na kumkamata.

Mtui alidai kuwa mbali na hayo pia hata haki za msingi kama vile kuswaki na kunywa chai, mbunge huyo ananyimwa na polisi, jambo ambalo ni ukiukaji mkubwa wa sheria ya mahabusu hapa nchini, ukilinganisha kuwa yeye bado ni mbunge na tena mwakilishi wa wananchi.

Alifafanua kuwa bado watakuwa na mbunge huyo na wataweza kufuata sheria za msingi, lakini kwa wale wote ambao wanamuonea mbunge huyo watachukuliwa sheria, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwani hali za uoneaji dhidi yake zinaongezeka siku hadi siku.

Kwa upande wa Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM mkoani Arusha, Isack Kapriano amelaani tukio hilo na kuiomba polisi kuhakikisha uchunguzi wa suala hilo unafanyika.

Naye Mulongo alipoulizwa juu ya Chadema kutaka kumfungulia kesi, alisema; “Huo ni upotoshwaji na naviachia vyombo vya uchunguzi kuendelea na uchunguzi wa jambo hilo, ikiwemo Lema kudai mimi nimemtumia ujumbe mfupi wa maneno wa kumbambikiza kesi.

“Sina la kuongeza, vyombo vya usalama vipo na vinafuatilia mambo haya hivyo nasubiri vifanye kazi zao, ikiwemo madai ya Lema dhidi yangu kwa SMS’’.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa saa tisa alfajiri, usiku wa kuamkia juzi, nyumbani kwake na kufikia jana aliendelea kuwa chini ya ulinzi, akihojiwa kuhusiana na vurugu zilizotokea katikati ya wiki hii katika Chuo cha Uhasibu Arusha baada ya mmoja wa wanafunzi wake, Henry Koga (22) kuuawa na watu wasiojulikana.

Anatarajiwa kufikishwa kortini kesho kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment