Enzi za uhai wa msanii Albert Mangwea R.I.P
Pretoria,Afrika Kusini
WAKATI taarifa ya kifo cha msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Albert Mangewea ikiendea kugubikwa na utata mwingi, baada ya taarifa za kifo chake kupingana kufuatia watoa taarifa hizo kutokuwa na vyanzo vya uhakika,Waandishi wameendelea kupata taarifa za kina juu ya kifo cha msanii huyo.
Akizungumza na Waandishi wa habari kwa njia ya simu akiwa Pretoria nchini Afrika msanii wa muziki wa kizazi kipya anayeishi nchini Afrika Kusini Bushoke amesema kwamba amesikia taarifa za kifo cha Mangwea lakini ahajaamini ingawa hapatikani kwenye simu yake.
Nilikuwa na mipango ya kukutana na Man Ngwea leo lakini nilipoa amka asubuhi nilijaribu kumtafuta kwenye simu yake sikumpata na kila nilipojaribu tena bado sikupata majibu yoyote, sikuwa na wasiwasi sana kwani nilidhani pengine simu haina chaji na angenitafuta baadaye"alisema Bushoke na kuongeza.:
"Niliendelea kumtafuta kwa zaidi ya saa nne ndipo nilipoanza kuwa na wasiwasi, kwani alikuwa na mipango ya kurudi Tanzania na kuna mambo mengi tulizungumza naye nikalazimika kumtafuta rafiki yake wakaribu lakini taarifa alionipa ilinishtua sana, jamaa aliniambia kwamba Man Ngwea amezimika".
Bushoke ambaye alikuwa rafiki wa karibu na msanii huyo alikzungumzia taarifa hizo kwa uchungu huku akiwa na kwi,kwi kila wakati alisema kwamba, anajiandaa kwenda Hospitali ya St. Hellen ya jijini Johanesburg ili akashuhudie kwa macho yake kama kweli Ngwea amefariki Dunia. Taarifa za kifo cha msanii huyo zimesambaa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania huku picha zake zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na nyimbo zake kupigwa kwenye vituo mbalimbali vya Redio.
No comments:
Post a Comment