Friday, 31 May 2013

Kinana ajipanga kumshitaki Tundu Lissu Mahakamani


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, akifafanua jambo

KATIBU Mkuu waChama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amenza kutekeleza moja ya majukumu yake ya kisiasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kukiangamiza  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Harakati za katibu Mkuu huyo wa CCM zimeanza kujulikana baada ya kuwepo kwa njama za kufufua kesi ya uchaguzi dhidi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),Tundu Lissu.
Njama hizo cha Kinana zimetangazwa leo na  Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa kufuatia kukamatwa kwa nyaraka zinazoonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CCM Kinana amewaelekeza waliokuwa mawakili wa makada wa CCM waliomfungulia Lissu kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki mwaka 2010 wafungue rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ili kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma iliyotupilia mbali kesi ya makada hao wa CCM dhidi ya Lissu.
Dk Slaa alisema kesi ya Mahakama Kuu ilitupiliwa mbali tarehe 27 Aprili mwaka jana huku akieleza kwamba lengo la njama za Kinana na CCM ni kuhakikisha kwamba Lissu anafutiwa Ubunge ili asiweze kushiriki katika mchakato wa Katiba Mpya kama mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba litakalojadili na kupitisha rasimu ya Katiba Mpya baadaye mwaka huu. “Kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge, Mheshimiwa Lissu amekuwa mwiba mkali kwa CCM na Serikali yake ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano. Amefumbua macho ya mamilioni ya Watanzania kuhusu masuala makubwa ya kikatiba na kisheria kwa hoja zake Bungeni"alisema Dk Slaa.
Alifafanua kwamba uelewa wake mpana wa masuala hayo na wa Kanuni za Bunge umekuwa kikwazo kikubwa kwa CCM na Serikali yake pamoja na uongozi wa Bunge kupitisha mambo yao kinyume cha sheria, Kanuni za Bunge na maslahi ya nchi, uwepo wake ndani ya Bunge na ujasiri wake katika kutetea hoja mbali mbali umemzuia Spika wa Bunge na uongozi mzima wa Bunge kuwaonea Wabunge wa Upinzani na hasa Chadema, Mtu huyu amekuwa adui mkubwa wa CCM ndio maana Kinana anataka aondolewe Bungeni ili asiwepo kabisa katika mjadala wa Katiba Mpya Bungeni.”

No comments:

Post a Comment