Rais wa Malawi Joyce Banda
MWANAFUNZI wa Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Phwezi ya wavulana nchini Malawi, Mathias Maweta (21) amehukumiwa kwenda jela miaka sita kwa kumlawiti mwanafunzi mwenzake. Maweta alihukumiwa jela kwa kumlawiti Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo mwenye umri wa miaka 14.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Rumphi Sophie Chimaliro pia aliamuru mwanafunzi huyo kupewa kazi ngumu katika kipindi chote atakachokuwa jela.
Mwendesha mashtaka Ofisa wa Polisi wa kituo cha Rumphi Malumbo Jere aliiambia Mahakama hiyo kwamba Mweta ambaye anatokea katika kijiji cha Mulumbe ,Zomba alimlawiti mwananfunzi mwenye umri wa 14 jina linahifadhiwa tarehe 27 Mei mwaka huu.
Kamanda Jere alisema kwamba mtuhumiwa alifaya kosa hilo majira ya saa 3:30 usiku katika viwanja vya mpira shuleni hapo. “Mtuhuiwa alimchukuwa kijana huyo mpaka kwenye viwanja vya mpira shuleni hapo bila kumweleza chochote, baadaye alianza kumlawiti huku akitishia kumpiga endapo angekataa kulawitiwa,kitendo kilichomfanya mtoto huyo aliye kwa uchungu" alisema Kamanda Jere.
Ofisa huyo wa Polisi alifafanua kwamba, baada ya Polisi kufika eneo la tukio walikuta Kondom za kiume zilizotumika na kuwafaya Polisi waamini kwamba mtuhumiwa alitumia Kondom hizo wakati wa kumlawiti mtoto huyo. Katika kutafuta ushahidi wa kina juu ya suala hilo Polisi pia walifanikiwa kupata baadhi ya Kondom katika begi la shule la mtuhumiwa huyo zilizo fanana na Kondoma zilizo okotwa uwanjani.
Hata uchunguzi wa madaktari uliofanywa katika Hospotali ya Wilaya ya Rumphi pia ulithibitisha kwamba kijana huyo alilawitiwa, mwendesha mashtaka huyo pia aliileza Mahakama hiyo kwamba mtoto huyo kwa hivi sasa anasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia tangu alipofanyiwa unyama huyo. Hata hivyo katika utetezi wake mtuhumiwa huyo aliiomba Mahakama hiyo imsamehe kwa sababu ni mwanafunzi na kwamba anatarajia kufanya mtihani wake wa mwishi juni 26 mwaka huu huku pia akieleza kwamba bado ana umri mdogo na angependa kuendelea na masomo yake. Hata hivyo hakimu wa Mahakama hiyo Chimaliro alisema kwamba hukumu itatekelezwa na kuwa fundisho kwa baadhi ya wanafunzi weye tabia ya kulawiti wanafunzi wenzao.
No comments:
Post a Comment