Sunday, 26 May 2013

Lady Jaydee, Lwakatale kuiteka Dar kesho........

 WAKATI kesi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare ikitarajiwa kusikilizwa kesho Mei 27 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kesi ya msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Judith Wambura (Lady JayDee) pia inatarajia kusikilizwa tarehemu hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kesi hizo zinatarajia kuvuta hisia za watanzania kutokana na mvuto na aina ya kesi hizo,Lwakatale atapanda kizimbani kwa mara nyingine huku akitarajia kupata dhamana ya kesi yake baada ya Mahakama Kuu kumfutia mashtaka ya Ugaidi yaliyokuwa yakimkabili awali na ambayo ilikuwa ikimnyika dhamana na kubaki na shitaka la kula njama ya kumdhuru Denis Msacky ambayo inadhaminika.
Kwa upande wa Lady JayDee anatarajia kupambanda kizimbani kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa hati ya mashtaka na kutakiwa kurudi mahakamani hapo kesho mei 27 .Waandishi wa habari walishuhudia barua kutoka mahakamani hapo pamoja na nyakara zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari zikiwamo blogu zilizoelezea ugomvi wake kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio Ruge Mutahaba.
“Hili ndilo shtaka lenyewe kwa hivyo sisi hatuwezi kusema chochote kwa sasa tunaelekea kwa mwanasheria wetu ili kuanza kuishughulikia kesi hii,” alisema Gadna Habash mume wa mwanamuziki huyo.
Kabla ya kufika mahakamani hapo mchana, mwanamuziki huyo alitoa mada katika jukwaa la sanaa Basata ambako alizungumzia changamoto nyingi zilizopo katika kufikia mafanikio kwenye sekta ya muziki.
Wakati kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Mei 27, siku nne baadaye Jaydee anasherehekea miaka yake 13 tangu aingie rasmi katika sekta ya muziki.

No comments:

Post a Comment