Sunday, 12 May 2013

MAHAUSIANO: KAMA MUMEO HUMFANYII HAYA UNAKOSEA!!!!

MAMBO MENGINE YA MSINGI:
*Penda kuuchunguza mwili mwako ili kuona kama ugonjwa wowote au la. Ni jambo linalokwaza, kuna wengine utashangaa kwamba mchana mzima hakusema kwamba anaumwa, lakini unapomwambia nahitaji hiki, ndipo naye anaanza kulalamikia aaah kichwa kinauma, aaah kiuno nk.
*Katika suala zima la maisha ya wanandoa, ni muhimu kupenda kuvaa nguo za kuvutia.
*Jiepushe kuonekana na mumeo ukiwa na nguo chafu au ukiwa ovyo.

*Jiepushe na mapambo yaliyokatazwa na mumeo. Ikiwa yeye hataki, unavaa kumfurahisha nani?
*Tumia aina ya manukano, rangi, na nguo ambazo mumeo anazipenda.
*Badilisha mtindo wa nywele, manukato n.k. mara kwa mara. Maana kuna wengine kama ni kusuka, basi kila mara ni aina moja tu ya nywele, sio sawa.
KUHUSU TENDO LA NDOA
*Harakisha kufanya tendo la ndoa mumeo anapokuwa na hamu ya tendo hilo. Ni makosa makubwa kulalamika kwa mfano aaah bwana eeeh nimechoka…jana nimekupa na leo unataka tena kwani mimi ng’ombe nk.
Kama ni kweli kuna tatizo, ni suala la msingi kuzungumza kama watu wazima kwa staha na sio kuongea kama mtu wa mitaani.
*Mnapokuwa katika uwanja wa mahaba, semeshaneni maneno ya mapenzi na mumeo. Acha kusema aaah sisi ni wazee au ni watu wazima. Mapenzi haya utu uzima.
*Mwache mumeo atosheleze hamu yake, wala hakuna sababu ya kupigishana makelele.
*Chagua wakati muwafaka na muda mzuri wa kumchangamsha mumeo, na kumtia hamu ya kufanya tendo hilo, mfano baada ya kurudi safari, mwisho wa wiki, n.k.

UMASKINI AU SHIDA NI MAPITO
Usiwe mnyonge kwa kuwa mumeo ni maskini au hana kazi nzuri ya kufanya. Cha msingi ni kuendelea kumuomba Mungu.
*Usimdai mumeo vitu vingi visivyo na ulazima au vile ambavyo unajua hana uwezo navyo.

No comments:

Post a Comment