Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai.
Alisema faida ya kuwapo kwa wabunge hao ni kuongezeka kwa uelewa, kitu ambacho kinafanya kila mtendaji wa Serikali kuwa makini, kwa kuwa wengi wao wana elimu ya kutosha ya kupambanua mambo.
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema hakuna kazi ngumu kama kuongoza Bunge hasa lenye wabunge vijana kama la kipindi hiki.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ndugai alisema
inamlazimu kufahamu historia ya kila mbunge, kwenda sambamba na
wanachotaka hasa wakati wa kujibizana.
Alisema hiyo ni changamoto kubwa, ambayo hata
watunga sheria wa Serikali wana wakati mgumu kuhakikisha kuwa wanakuwa
makini kutokana na kuongezeka kwa changamoto
.
.
Alisema faida ya kuwapo kwa wabunge hao ni
kuongezeka kwa uelewa, kitu ambacho kinafanya kila mtendaji wa Serikali
kuwa makini, kwa kuwa wengi wao wana elimu ya kutosha ya kupambanua
mambo.
Ndugai aliutaja upungufu wa kuwapo kwa wabunge
vijana kuwa ni kutaka mambo kwa haraka, ambapo wakati mwingine kabla
hawajasikiliza kinachosemwa wanakuwa wamedakia kujibu na kupoteza maana
nzima ya kuwa na sehemu ya kusikiliza matatizo na kuyafanyia kazi.
“Kuna wakati inanilazimu kuwapa majibu ya papo kwa
hapo kulingana na jinsi ninavyowaelewa, ili kuwatuliza halafu baadaye
nikipata nafasi nakaa nao,” alisema.
No comments:
Post a Comment