Ni kuhusu chenji za rada. Mmoja asema zimetumika , lakini mwingine akataa.
Dodoma. Manaibu Waziri wiwili jana walipishana katika majibu yao kuhusu fedha za rada na kujikuta wakitoa majibu tofauti hali iliyowachanganya wabunge na kusababisha baadhi kuomba mwongozo.
Hali hiyo ilitokea ndani ya Bunge baada ya Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene kueleza kuwa fedha za rada hazijagawanywa kwa kuwa bado kuna taratibu ambazo zinatakiwa kufanyika.
Mbene alitoa kauli hiyo kufuatia swali la nyongeza la Moses Machali aliyetaka maelezo kuhusu tetesi kuwa ziko kampuni ambazo zimepewa tenda ya kununua vitabu na madawati.
“Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la mbunge kama ifuatavyo, hadi sasa fedha hiyo haijagawanywa kwani bado kuna mambo ambayo yanahitaji kukamilishwa,” alisema Mbene.
Kutokana na majibu hayo, ilimlazimu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa kusimama na kulieleza Bunge kuwa fedha hizo tayari zimeshagawanywa na kuanza kufanya kazi.
Majaliwa alisema kati ya fedha hizo, Sh 55.2 bilioni zimepangwa kununua vitabu kwa Tanzania Bara, na Sh 18 bilioni zitanunua madawati tenda ambazo zimetolewa kwa kampuni tisa.
Suala hilo linajitokeza baada ya mkutano uliopita kuidhinisha matumizi ya fedha hizo kwamba zitumike katika kuboresha elimu pekee.
Awali Mbunge wa Nungwi Yusufu Haji Khamisi (CUF) alitaka kujua Sekta ya elimu Zanzibar imetengewa kiasi gani kutoka fedha za rada.
No comments:
Post a Comment