Vijana ni lazima wawe na mawazo ya kujitegemea kwa kuanzisha miradi mbalimbali ndipo Serikali inaweza kuwasaidia. Ninapokutana na vijana ambao wamejikusanya na kuanzisha mradi kwa lengo la kujiajiri ninafarijika kuchangia fedha ili kuwaongezea nguvu.”
Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa chama Chama mapinduzi.
Morogoro. Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kujitathmini kwa kuwatembelea wananchi na wanachama wake kuangalia uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani yake ya 2010-2015.
Ziara zinaongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ambaye wiki iliyokwisha alimaliza ziara ya siku nane katika Mkoa wa Morogoro.
Morogoro ni mkoa sita kutembelewa na Kinana, tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo Novemba mwaka jana. Tayari amefanya ziara ya namna hiyo katika mikoa ya Mtwara, Rukwa, Geita, Arusha na Kigoma.
Akiwa Morogoro, Kinana alitembelea wilaya sita zinazounda mkoa huo – Kilosa, Kilombero, Ulanga, Gairo, Mvomero, Morogoro Vijijini na Morogoro Mjini.
Uhai wa chama
Morogoro ni miongoni mwa ngome zinazotegemewa na CCM kwani majimbo yote 10 ya uchaguzi yaliyopo katika mkoa yanashikiliwa na CCM. Pia kati ya kata 181 zilizopo mkoani humo, ni chache tu zinazoshikiliwa na vyama vya upinzani.

Hata unapopita katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro, bendera za kijani zinatawala huku bendera chache za Chadema na CUF zikiwa zinaonekana kupepea.
Katika mkoa huo, Kinana amefungua mashina ya wakereketwa 50 kwa niaba ya mengine zaidi ya 400. Katika mashina hayo, kila shina lilikuwa na idadi ya wanachama wapya kati ya 30 na 70.
Ingawa takwimu halisi za wanachama wapya katika mkoa huo bado hazijapatikana lakini kuna wananchi wengi wamejiunga na chama hicho.
Ingawa takwimu halisi za wanachama wapya katika mkoa huo bado hazijapatikana lakini kuna wananchi wengi wamejiunga na chama hicho.
CCM inaonyesha imebadili mbinu ya siasa zake kwa kuyafanya mashina kuwa vikundi vya kujiendeleza kiuchumi badala kuwa vijiwe vya kupika majungu.
Hata risala alizosomewa katika mashina hayo, vijana wakereketwa walielezea miradi wanayoifanya na Kinana akawaongezea ahadi za kuwasaidia ili waweze kufanikisha miradi hiyo.
Hata risala alizosomewa katika mashina hayo, vijana wakereketwa walielezea miradi wanayoifanya na Kinana akawaongezea ahadi za kuwasaidia ili waweze kufanikisha miradi hiyo.
Kinana anasema vijana ni lazima wawe na mawazo ya kujitegemea kwa kuanzisha miradi mbalimbali ndipo Serikali inaweza kuwasaidia. “Ninapokutana na vijana ambao wamejikusanya na kuanzisha mradi kwa lengo la kujiajiri ninafarijika kuchangia fedha ili kuwaongezea nguvu,” anasema Kinana.
Katika mashina mengi ya wakereketwa, Kinana aliahidi fedha, vifaa ili miradi yao iweze kufanikiwa
Moja ya miradi ambayo mashina ya wakereketwa wengi walionyesha kuvutiwa nayo ni mradi wa pikipiki, maarufu kama bodaboda.
Katika ziara hiyo, wananchi mbalimbali wakiwamo viongozi walitangaza kujitoa katika vyama vya upinzani na kujiunga na CCM.
Katika ziara hiyo, wananchi mbalimbali wakiwamo viongozi walitangaza kujitoa katika vyama vya upinzani na kujiunga na CCM.
Miongoni mwao ni Mwenyekiti wa Chadema katika Kata ya Kiroka, Shaaban Mponda na Mwenyekiti wa CUF wa kata hiyo, Adimu Omar ambao walimkabidhi Kinana kadi zao.
Viongozi hao baada ya kujiunga na CCM wamesema wataendelea kuwahamasisha wanachama wa vyama vya upinzani kujiunga na CCM
Viongozi hao baada ya kujiunga na CCM wamesema wataendelea kuwahamasisha wanachama wa vyama vya upinzani kujiunga na CCM
Mponda anasema kuwa amekuwa akiwahamasisha wana Chadema kujiunga na chama hicho.
“Nilikuwa najitolea kusafiri kwa baiskeli kwenda vijijini kuingiza wanachama wapya, hawa nitawahamasisha kujiunga na CCM,” anasema Mponda.
“Nilikuwa najitolea kusafiri kwa baiskeli kwenda vijijini kuingiza wanachama wapya, hawa nitawahamasisha kujiunga na CCM,” anasema Mponda.
futa sehemu ya comments
ReplyDelete