Friday 3 May 2013

MBOGA ZA MAJANI MLO KAMILI WA MTOTO:NJEGERE NA MSUSA..



Leo asubuhi nilipokua hosipitali nimejikuta nikimgombeza mama mmoja aliyekua amebeba mtoto mwenye afya mbaya na dhoofu alafu anawasema vibaya watoto  wa mama mwingine ambao  ni wanene. Naomba nirudie maneno yake”HAO WATOTO MABONGE SANA,EHH!MATAJIRI  WANAJIDAI KUWAPA WATOTO MANYAMA,MAKUKU,MAYAI NA MACHAKULA YA KIZUNGU,SASA ONA EHH”…hakujua tu ambavyo nilikua namshangaa huyo wakwake alivyo na afya mbaya,na kwasababu maneno yake yalinikera, basi akawa amenipa sababu yakumsema yeye mwenyewe juu ya afya ya mwanae.Na nilipomsema sana  akaniambia yeye hawezi nunua hivyo vyakula vya kitajiri.
Jamani  kina mama,kumpa mtoto lishe bora haina maana mpe nyama au samaki kila siku,wala haimaanishi  apate uji wenye mayai kila siku.
Kwenye makala za nyuma nimeongea sana kuhusu virutubisho muhimu kwa mtoto na kukwambia ambavyo virutubisho hivyo huusika sana na ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili.Pia nimeongea sana kuhusu lishe bora (balanced diet)Kama umesoma makala hizo kwa umakini utakua umegundua umuhim wa mboga za majani kwenye lishe ya mtoto.
Nirudie tena leo,Mboga za majani hubeba virutubisho vingi muhimu.Mtoto anaweza kua na afya nzuri tu hata asipopata nyama,kuku na mayai.Hivyo virutubisho vyote unavyotafuta kwenye nyama,kuku,mayai vinapatikana kwenye mboga za majani.
Naomba muache kutafuta sababu za kutowapa watoto lishe bora,Acha kabisa kusingizia gharama kubwa za nyama na kuku,njegere na majani ya maboga pia vinafaa.
Mahitaji
Njegere  Nusu kikombe
Nyanya 2
Vitunguu maji 2
Karoti 2
Hoho 2
Msusa/majani ya maboga vikombe 2 (yanatakiwa kua mengi)
Makaroni  kikombe kimoja
Maziwa  fresh vikombe 2
Blue band kijiko kimoja cha chakula
Chumvi kidogo
Njia
1.Chemsha makatoni,yakiiva weka pembeni
2.Osha,menya,kata mboga zote za majani.
3.katika sufuria weka njegere,nyanya,hoho,vitunguu na hoho,ongeza maji  vikombe viwili kisha funika na  bandika jikoni.Chemsha adi maji yabaki kidogo(lazima vitakua vinaelekea kuiva)
 
4.Ongeza maKaroni kwa juu ,usigeuze wala kuchanganya.
2013-03-25 11.08.24 
5.Ongeza maziwa kisha acha yachemke,usigeuze wala kuchanganya  na usifunike sufuria.
2013-03-25 11.09.47 
6.Maziwa yakichemka ongeza blue band na chumvi.
2013-03-25 11.14.15 
7.Ongeza Majani ya maboga,kisha punguza kabisa moto uwe mdogo kama wakubanikia wali.Funika sufuria kisha acha kwa muda ili  majani ya maboga yaive.
2013-03-25 11.15.42 
  • Hakikisha majani ya maboga hayaivi sana
  • Lengo la kupunguza moto ni kutaka majani ya maboga yaive kwa joto dogo na taratibu ili kutunza virutubisho vyake na pia kuhakikisha fiber(nyuzinyuzi)hazilainiki.
  • Kama umesoma makala niliyoandika miezi ya nyuma juu ya lishe ya mtoto mdogo naamini utakua umegundua kwamba mboga zenye rangi ya kijani iliyokooza zinabeba virutubisho vingi ambavyo ni muhim kwa mtoto.
8.Adi apo chakula kimeiva.Acha chakula kipoe kikiwa kimefunikwa,usifunue kabisa chakula hiki.
  • Lengo la kutokukifunua ni kutunza joto la chakula ili joto hilo liendelee kuivisha chakula hicho.Upishi wa chakula hiki ni wa moto mdogo na kwa muda mfupi hivyo kunakilasababu ya kuendelea kuivisha kwa joto hilo.
9.Chakula kikipoa ,unaweza kusaga kama mtoto bado ni wakula chakula cha kusaga.
2013-03-25 11.18.13 
  • Hata baada ya kusaga chakula hiki,hakitakua laini kama mtori,kitabaki kua na nyuzinyuzi  ndogondogo ambazo ni nzuri kwa mtoto.Zinasaidia sana kuwezesha digestion ya chakula kwa mtoto.
Ni vyema sana  ukajitaidi kuongeza mboga za majani za aina mbalimbali kwenye lishe ya mtoto kwani Mboga za majani zina virutubisho vingi.
Unaweza kuchanganya mboga zozote unazopenda,naomba usisahau kwamba ubora wa chakula si virutubisho tu,ladha pia inahusika.hakikicha chakula kinakua na ladha nzuri ili mtoto afuraie.




No comments:

Post a Comment