Friday 3 May 2013

NYANYACHUNGU ZILIZOPIKWA NA KARANGA-Namna nyingine ya kumfanya mtoto ale mboga za majani...

035

Kila ninapopika au kula nyanya chungu za karanga namkumbuka na kummiss marehem Bibi yangu,mzaa baba yangu.Bibi alikua anapenda saana mboga za majani.Alipenda zaidi  nyanyachungu,lakini alidai kwamba mboga hiyo ni chungu ndio maana anapoipika lazima aongeze karanga ili kuipa ladha nzuri.
Nakumbuka kila tulipokwenda likizo kumsalimia ,Mama alimtengenezea Bibi karanga  za kusaga kwa ajili ya kupikia mboga za majani.
Mboga za majani zenye karanga hupendwa sana na watoto,kwani wanafuraia ladha ya karanga,na hawasikii ile ladha ya mboga wasiyoipenda.
Recipie hii ya kupika nyanyachungu ni maboresho ya recipie  ya Bibi.
029 
Mahitaji
  • Nyanyachungu robo kilo
  • vitunguu maji 2 Vikubwa
  • vitunguu swaumu kijiko 1 cha chakula
  • nyanya 3 kubwa
  • nyanya ya kopo kijiko kimoja 1 cha chakula
  • hoho 1 kubwa
  • karoti 1 kubwa
  • karanga zilizosagwa au kusiginwa nusu kikombe
  • Mafuta ya kula vijiko 2 vya chakula
  • chumvi kwa kiasi unachopenda
  • 001 
Njia
1.Osha,katakata nyanya,hoho,karoti,na vitunguu swaumu na kisha weka kwenye mashine ya kusagia juice(blender au food processer),ongeza robo kikombe cha maji na uvisage pamoja.
005 (2) 006 (2) 
2.Osha,menya na ukate kila nyanyachungu katika vipande vinne kwa urefu.
3.chukua karanga zilizokaangwa na kisha saga kwenye mashine ya kusagia karanga kama unayo,kama huna nunua unga wa karangaaua karaga iliyosiginwa.baada aya kupata unga wa karanga au karanga iliyosiginwa,weka maji nusu kikombe na karanga hizo kwenye mashine ya kusagia juisi(blender)kisha usage pamoja,ili kuzichanganya na kutengeneza uji mzito wa karanga.
007  008 
4.Menya,osha,kata kitunguu maji.Weka mafuta kwenye sufuria kisha ongeza kitunguu na ukaange adi kitunguu kianze kubadilika rangi,usiache kitunguu kiwe cha brauni.Ongeza mchanganyiko wa nyanya(maelekezo namba moja),nyanya ya kopo na nyanya chungu kwa wakati mmoja.
010 (2) 012 (2) 
014 (2) 
  • Lengo la kuweka mchanganyiko wa nyanya za kusaga na nyanyachungu kwa pamoja ni ili kuivisha nyanya chungu kwa kutumia nyanya bila kuongeza maji.
5.Geuza vizuri ili kuchanganya ,kisha funika na uache ziive.Guza mara kwa mara ili zisiungue chini.ivisha adi nyanya zikauke
018 
6.Mimina uji wa karanga(maelekezo namba 3) juu ya nyanyachungu kisha ongeza chumvi na ufunike viiv.usikoroge au kuchanganya karanga.hakikisha moto wako si mkali pale unapoweka karanga kwani karanga hushika chini na kuungua kwa haraka.
019 (2) 022 
7.Ukiona karanga zimeshika moto na zinatokota,anza kugeuza ili zisiungue,pika ukigeuza adi karanga iive na maji yakauke.Inatakiwa kua nzito na ishikane na nyanyachungu.Tafadhali zingatia muonekano huu katika picha,hapa chini.
024 
Mboga tayari kwa lunch au dinner.Mimi niliitumia kwa ajili ya chakula cha mchana,na niliisindikiza kwa ugali na matango pembeni.
Ipe familia yako chakula kilichobora.



No comments:

Post a Comment