Tuesday, 28 May 2013

Mwanafunzi Chuo Kikuu azalia hostel............

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu kimoja kilichopo katika mji wa Eldoret nchini Kenya amejifungua mtoto kwenye chumba cha mpenzi wake, mwanafunzi huyo aliyekuwa mwaka wa kwanza alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi aliyekuwa chuoni hapo kwa muda.
Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na furaha sana alipojua kuwa ni mjamzito na aliwaambia rafiki zake, baada ya kumaliza mwaka wa kwanza wa masomo yake Novemba mwaka jana alirudi nyumbani kwa likizo ndefu na kumuacha mpenzi wake ambaye alikuwa bado anaendelea na masomo yake.
Imekuwa ni kawaida kwa vyuo vikuu vingi wanaume kubadilisha wasichana na kuwaacha wapenzi wao, ambao wanakuwa wanatarajia kupata watoto na hivyo kurudi vijijini kwao.Wazazi wengi wanakuwa na wasiwasi na jinsi ya kuwalinda wajukuu zao, kwani wanafunzi wengi wamekuwa wakipata mimba na hao wanaowapa mimba hawatunzi ujauzito wala kutoa huduma kwa watoto wanaozaliwa.
Wasichana wanapojaribu kupiga simu kwa wanaume ambao wamewapa ujauzito huwa hawapokei simu, wazazi wanapoona hakuna mahitaji yoyote kutoka kwa wanaume waliowapa ujauzito wanawambia watoto wao waende kumuangalia, wazazi wanaona hakuna njia nyingine ila ni kumwambia mtoto wao aende chuo ili kumuangalia mwanaume huyo aliyempa ujauzito, kwa sababu hata akimpigia simu hapokei. Kwa upande binti huyo ambaye jina lake halifahamika mara moja alikuwa na bahati kwani mwenye bimba hiyo hakuwahi kubadili makazi na inakuwa ni rahisi kwenda kwenye chumba chake na kumuona mwanaume huyo, alipoigia ndani akiwa na uso wa huzuni jamaa huyo aliamua kumuacha akae kwenye chumba chake  ila kadri muda ulivyozidi kwenda msichana alijikuta ameshafikia hatua ya kujifungua.

No comments:

Post a Comment