Saturday, 4 May 2013

Mwanamume akikosa mtoto hupata huzuni zaidi kuliko mwanamke....




DONDOO MUHIMU
Utafiti ulihusisha watu 108, kati yao 27 walikuwa wanaume na  81 wanawake.Ulifanyika kwa kukusanya maoni katika mtandao, midahalo na kujaza madodoso.Walioshiriki walikuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 66.
Wenye umri usiopungua miaka 41 ndiyo walijibu maswali hayo.Waliosema wanahitaji watoto
Wanaume asilimia 59 na wanawake ni asilimia 63.
Sababu  za kutaka watoto
Asilimia 38 ya wanaume walihitaji mtoto kwa kuwa hawakuwa na mtoto kabisa, huku asilimia 27 tu ya wanawake ndiyo walikuwa hawana watoto kabisa.
Idadi ya wasio na watoto
Kati ya kila wanaume wanne  mmoja hana kabisa mtoto, ikilinganishwa na asilimia 18 ya wanawake ambao hawana watoto.
Utafiti huo umebainisha kuwa asilimia 55 tu ya wanaume ndiyo walikuwa wanataka kuongeza watoto, ukilinganisha na asilimia 59 ya wanawake ambao walikuwa wanahitaji kuongeza.Utafiti mdogo uliohusisha wanawake na wanaume 125 ambao tayari wana watoto unaonyesha kuwa pamoja na wanaume kupata madhara bado hawapendi kuwa na watoto wengi kama wanawake. Wataalamu wa Saikolojia Tanzania waunga mkono matokeo ya utafiti huo.
Tofauti na mazoea na mtazamo wa wengi kwamba mwanamke ndiye anayeumia zaidi akikosa mtoto, wataalamu wamegundua kuwa anayeumia zaidi kwa kukosa mtoto ni mwanamume.
Utafiti huo umeonyesha kuwa wanaume wanahitaji mtoto sawa sawa na wanavyohitaji wanawake, lakini wao wanaumia zaidi wanapokosa bahati ya kupata mtoto.
Wataalamu hao wamebaini kuwa sababu kubwa zinazowafanya wanaume wajisikie vibaya zaidi wanapokosa watoto ni tamaduni za toka enzi kuwa wao wanaweza kila kitu na msukumo wa familia.
Tofauti na wanawake, ambao wanahitaji mtoto kwa ajili yao binafsi kwa asili ya kuumbwa kwao, hali ambayo kitaalamu inajulikana kama ‘biological urge’.
Taarifa za utafiti huo ulioongozwa na Robin Hadley, wa Chuo Kikuu cha  Keele, ukishirikisha wanaume 27 na wanawake 81, ambao hawajapata mtoto, uliwasilishwa mbele ya Wanasaikolojia wa Taasisi ya British Sociological Association,  ya Uingereza.
Waohitaji zaidi watoto
Kwa idadi hiyo waliosema wanahitaji watoto ni wanaume asilimia 59 na wanawake ni asilimia 63.
Nusu ya wanaume walisema kukosa mtoto kunawafanya waonekane tofauti kwenye jamii, huku wanawake wakisema wanahitaji watoto ili waje kuwasaidia baadaye.
Utafiti huo ulibaini kuwa asilimia 38 ya wanaume walihitaji mtoto kwa kuwa hawakuwa na mtoto kabisa, huku asilimia 27 tu ya wanawake ndiyo walikuwa hawana watoto kabisa.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa wanaume wanajisikia vibaya zaidi kukosa watoto kwa sababu asilimia ya wasio na watoto ni wanaume,tofauti na wanawake ambao wakati mwingine hubahatika kupata mmoja au wawili.
Tafiti hizo zilionyesha kuwa kati ya kila wanaume wanne  mmoja hana kabisa mtoto ikilinganishwa na asilimia 18 ya wanawake ambao hawana watoto.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa asilimia 56 ya wanaume hawana watoto kabisa, ikilinganishwa na asilimia 43 ya wanawake ambao hawana.
Akizungumzia utafiti wake Dk Hadley, anaeleza kwamba  amegundua kuwa kati ya wazazi wawili aliye kwenye hatari ya kukosa mtoto kabisa ni mwanaume, huku akiumia zaidi anapopatwa na hali hiyo kiasi cha kuwa na hasira, kujisikia vibaya mbele za watu, kujitenga na jamii, kuwa na wivu na mambo yanayofanana na hayo.
Wanawake kupenda watoto
Anabainisha kuwa hiyo ndiyo sababu inayowafanya wanawake wapende kupata watoto kuliko wanaume ili kuwaondoa kwenye matatizo hayo, ambayo mara nyingi husababisha familia nyingi kusambaratika bila kujali zilikuwa kwenye maelewano ya kiasi gani.
Alisema kwamba utafiti huo ulifanyika kwa njia ya kukusanya maoni kwenye mtandao, midahalo, kujaza dodoso za majibu na ulihusisha watu wenye umri wa kati ya miaka 20-66 huku wengi waliojibu maswali hayo walikuwa na umri usiopungua miaka 41.

No comments:

Post a Comment