SERIKALI ya Chama Cha Mapinduzi inadaiwa kuandaa mazingira ya kumwongezea Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda wa kuongoza nchi.
Taarifa za kuwepo kwa maandalizi hayo yalifichuliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Haruna Ibrahim Lipumba ambaye alisema kwamba Serikali inajiandaa kupeleka hoja hiyo Bungeni ili wabunge wa CCM ambao ndiyo wengi Bungeni waipitishe kwa kauli moja.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha Baraza jijini Dar es Salaam Profesa Ibrahimu Lipumba alidai kuwa amenasa taarifa za siri za kuwapo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ili iendelee kukaa madarakani hadi mwaka 2017.
Profesa Lipumba alisema hatua hiyo ya Serikali inakuja baada ya wasiwasi wa mchakato wa Katiba Mpya kutokamilika mwaka 2014 kama ilivyokuwa imepangwa awali na kufanya uchaguzi mwaka 2015 kushindika chini ya Katiba Mpya kama ilivyopangwa.
Profesa Lipumba alisema kuwa Serikali inataka kuongezewa muda wa kukaa madarakani kwa miaka miwili ikimaanisha kuwa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete itakaa madarakani hadi mwaka 2017 itakapo kamilisha mchakato wa katiba hiyo..
No comments:
Post a Comment